Mambo ya kufanya wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka

Zahara Tunda 2342Hrs   Disemba 23, 2018 Maoni & Uchambuzi
  • Tembelea ndugu, jamaa na marafiki ili kudumisha mahusiano ya familia.
  • Toboa mfuko nenda sehemu za kupumzisha akili yako ili uweze kutafakari yajayo.
  • Kipindi hiki ni cha kujitafakari wapi ulipotoka, wapi unakwenda na nini matarajio yako ya baadaye.

Kipindi cha mwisho wa mwaka kimezoeleka kuwa cha mapumziko sehemu mbalimbali duniani kutokana na uwepo wa sikukuu za krismasi na mwaka mpya.

Wakati huu pia hutumika na watu kutafakari walichofanya kwa mwaka mzima na kujipanga namna ya kufanya vema zaidi katika mwaka mpya. Lakini kila mtu huwa na namna anayofanya ili kuweza kufurahia vizuri uwepo wa mapumziko hayo.

Baadhi ya makabila wamekuwa na tabia ya kurudi vijijini kwao kwenda kusheherekea na kupanga mambo mbalimbali ya kiukoo kwa mwaka unafuata.

Hata hivyo, kama upo tu nyumbani na hujui ufanye nini kipindi hiki cha mapumziko ukiondoa kulala na kuangalia televisheni, Nukta inakuletea mambo muhimu unayoweza kufanya ili kuchangamsha akili na kujiandaa na mwaka mpya.


Tembelea vivutio vya kitalii

Tembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii ili kuangalia na kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitakupa burudani na kukupa ahueni baada ya mapambano ya mwaka mzima.

Kwa mkazi wa Dar es Salaam unaweza kwenda hata kutembelea bustani ya wanyama ya Dar es Salaam Zoo iliyopo Kigamboni ukiwa na familia yako kuangalia wanyama na kufurahia michezo mingine ya watoto.

Bagamoyo pia si mbali na Dar es Salaam kule utajifunza historia ya watumwa, utaona kaburi la wapendanao, na majengo mbalimbali ya zamani yenye historia kedekede. Kuliko kulala siku nzima nyumbani fanya mpango wa kujitoa na ukajifunze.

Wakati huu wa mapumziko unaweza kuutumia vizuri kwa kuhakikisha upo karibu na watoto wako kwa kushiriki kucheza nao na kutoka nao 'outing’ (matembezi) kidogo.

Tumia muda wako kuwapeleka watoto maeneo mbalimbali ya michezo kama Fun City, Mlimani City, Quality Center na kwingineko waende wakafurahie na watoto wenzao. Katika outing hizo wewe kama mzazi unaweza muda mzuri wa kumsoma mwanao vitu anavyovipenda.

Hiyo itakusaidia kufahamu mategemeo aliyonayo kwa maisha yake ya baadaye na jinsi ya kumsaidia kufikia ndoto  zake.

Michezo ambayo watoto wanaifurahia wakiwa na wenzao hivyo ni muhimu kwa mzazi kipindi hiki cha mapumziko kuangalia namna ya kumfanya mwanao awe na furaha. Picha|FunCity


Ipe familia muda wako

Mwaka mzima ulikuwa na pilikapilika za kazi kuhakikisha maisha yanaenda. Kwa wale ambao hawana watoto au bado hawajaingia kwenye ndoa ni wakati mzuri wa kwenda kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki ili kudumisha upendo. 

Hili pia linawahusu wazazi wenye watoto, huenda mwaka mzima walibanwa na kazi na kushinda kuwa karibu na familia zao. Kipindi hiki ambacho wengi wako likizo ni muda sahihi wa kukaa na familia kujadili mambo muhimu yanayoweza kuimarisha uhusiano na upendo wa familia.

Mapumziko hayo mnaweza kuyafanya nyumbani kwa kufanya shughuli za usafi, kupika hata kucheza pamoja. Lakini kama mnataka eneo tulivu mnaweza kutoka na kwenda kijijini au maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya familia.


Zinazohusiana: Jinsi ya kufanya mitandao ya kijamii isikuharibie mahusiano yako

                           Utaoa, utaolewa lini: Jinsi unavyoweza kukabiliana na msukumo wa nje wa ndoa



Tafakari yajayo ukiwa maeneo tulivu

Nenda maeneo ya ufukweni na kama una vuwezo kodi chumba cha hoteli yenye utilivu na kaa ujitafakari ukiwa katika sehemu zuri na yenye upepo mwanana. Haya mambo siyo ya wazungu tu hata sisi tunaweza kama tukijiwekea utamaduni huo.

Na wale wanaokaa maeneo karibu na bahari, maziwa, au mito ambayo pembeni kuna hoteli za kisasa nenda kujitoa siku mojamoja sio mbaya, ila angalia sana bajeti yako usije kutumia hadi bajeti yako ya Januari.

Hata hivyo, kuna baadhi ya fukwe hazihitaji kuwa na pesa nyingi na zingine ni za bure. Basi tumia muda wako vizuri, nenda kafurahie beba ndugu au marafiki mkafurahie kwa pamoja, kwa sababu maisha yenyewe ni hayahaya.

Mapumziko ni pamoja kutumia muda wako na familia kutafakari mahusiano yenu na jinsi ya kuboresha. Picha| Shutterstock


Pumzika kwa kulisha ubongo maarifa mapya

Kwa mpenzi wa vitabu basi muda huu unaweza tafuta kitabu kimoja cha kufungia mwaka.Soma kwa makini ukielewe na uweze kuburudika kwasababu kazi ya mapumziko ni kufurahi hivyo hakikisha unafanya vitu vinavyokufurahisha.

Lakini kumbuka mwisho wa mwaka ndiyo ni ufunguo wa mwaka mpya, umejipangaje kuzikabili changamoto na kutekeleza malengo yako?

Related Post