Mambo 10 yaliyotokea duniani kwa mara ya kwanza 2021

December 16, 2021 5:41 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Samia Suluhu Hassan kuwa raia wa kwanza mwanamke Tanzania.
  • Kuvumbuliwa kwa bahari mpya ya tano.

Dar es Salaam. Kila mwaka dunia inashuhudia mambo mapya ambayo yanaingia katika kumbukumbu za dunia kutokana na umuhimu wake hasa katika maendeleo ya dunia.

Matukio hayo huwa mabaya au mazuri lakini huacha somo muhimu kwa watu na namna wanavyohusiana katika mazingira wanayoishi. Haya ndiyo mambo 10 yaliyotokea mwaka huu kwa mara ya kwanza:

1. Tanzania yapata Rais wa kwanza mwanamke

Nchi ya Tanzania iliyopo Afrika Mashariki Machi 17, 2021 ilimteua Samia Suluhu Hassan kuwa rais wake wa kwanza mwanamke tangu ilipopata uhuru mwaka 1961.

Kabla ya kushika wadhifa huo, Rais Samia alikuwa Makamu wa Rais tangu 2015 katika Serikali ya awamu ya tano iliyokuwa inaongozwa na Hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 kutokana na matatizo ya moyo. Magufuli pia alikuwa rais wa kwanza kufariki akiwa madarakani Tanzania.

Samia ambaye atashikilia wadhifa wa urais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wa urais mpaka 2025, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini. 

 Aina ya kuchukua hatamu kwa Samia ambaye anakuwa rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar imetokea kwa mara ya kwanza, yaani kwa rais kufariki akiwa madarakani na makamu wake kuchukua nafasi.

Rais Samia Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride baada ya kuapishwa Machi 19, 2021. Picha| Reuters.

2. Mwanamke Mwafrika anaongoza Shirika la Biashara Duniani

Dk Ngozi Okonjo-Iweala aliweka historia mwezi Machi kwa kuwa Mwafrika wa kwanza na mwanamke wa kwanza kuhudumu kama mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Dk Okonjo-Iweala pia alikuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu kama waziri wa fedha katika nchi yake ya asili ya Nigeria, nafasi ambayo alishikilia mara mbili.

Dk Okonjo-Iweala ambaye ni gwiji wa uchumi alichukua nafasi ya mtangulizi wake Roberto Azevêdo aliyetangaza kuachia wadhifa huo mwaka mmoja kabla ya kumaliza kipindi chake.

Azevedo aliachia rasmi kiti hicho Agosti 31 mwaka jana.

Kuteuliwa kwa mtaalam huyo wa uchumi kushika nafasi ya juu ya WTO ni muendelezo wa viongozi wa dunia kutambua uwezo na nafasi ya mwanamke kulete maendeleo duniani. 

Miongoni mwa wanawake wanaoshika nafasi za juu ni Kristalina Georgieva kutoka Bolivia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) huku Kamala Harris akichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Marekani baada ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2020. 

Dk Ngozi Okonjo-Iweala mwenye taaluma ya uchumi amehudumu katika taasisi mbalimbali duniani kabla ya kuwa bosi wa Shirika la Biashara Duniani. Picha| Times. 

3. Ubongo wa mwanadamu waunganishwa bila waya kwenye kompyuta

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Brown cha Marekani mwezi Aprili waliunganisha kikamilifu ubongo wa binadamu kwenye kompyuta kupitia kifaa cha kupitisha sauti.

Hiyo ilikuwa ni jaribio la kuboresha matibabu kwa watu waliopooza ili kuwawezesha kurudi katika hali ya kawaida.

Washiriki wa jaribio hilo waliopooza waliweza kusogeza viungo vya roboti kwa kufikiria tu mienendo yao.

4. Wachora ramani za National Geographic wanatambua bahari ya tano ya dunia

Katika Siku ya Bahari Duniani Juni 8, Jumuiya ya Kitaifa ya Kijiografia ilitambua rasmi eneo la kasi la sasa linalozunguka Antaktika kama Bahari ya Kusini. 

Shirika hilo, ambalo limekuwa likichapisha ramani na atlasi tangu 1915, limechora ramani mpya inayokubali maji, ambayo wanasayansi na watafiti kwa miaka mingi walikuwa wanaitofautisha na bahari ya Atlantiki, Pasifiki, Hindi na Arctic.


5. Richard Branson, raia wa kwanza kuingia angani kwa chombo chake binafsi 

Katika hatua kubwa kuelekea kufanya utalii wa nyota kuwa ukweli, mwanzilishi wa kampuni ya Virgin Galactic, Branson alishinda mbio za anga za mabilionea, akiruka angani Julai akiwa ndani ya  chombo cha SpaceShipTwo chenye mabawa kilichotengenezwa na kampuni yake. 

Siku tisa baadaye, Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon na Blue Origin, alijiunga na klabu ya anga ya mabilionea katika roketi yake, New Shepard. 


Soma zaidi:


6. Shule ya kwanza duniani ya teknolojia ya 3-D yafunguliwa Malawi

Shule ya kwanza duniani ya teknolojia ya 3-D ilifungua milango yake mwezi Julai nchini Malawi. Shule hiyo ilijengwa na 14Trees kwa ubia kati ya kampuni ya maendeleo ya Uingereza na kampuni ya Uswisi inayojishughulisha na vifaa vya ujenzi. 

Teknolojia hiyo inasaidia kukabiliana na upungufu wa madarasa na shule kwa sababu wanafunzi wanaweza kusoma sehemu salama isiyohitaji vyumba vingi.

Shule iliyojengwa kwa teknolojia ya 3-D nchini Malawi. Picha| Mtandao.

7. El Salvador inakuwa nchi ya kwanza kufanya Bitcoin kuwa sarafu ya Taifa

El Salvador ilipitisha sheria mnamo Septemba ya kuifanya sarafu ya kidijitali ya Bitcoin kama sarafu halali ya Taifa hilo pamoja na dola ya Marekani. 

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa nchi hiyo hawakubaliani na uamuzi huo kwa sababu sarafu hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimfumo.

Wataalamu wa masuala ya fedha walisema kuwa sarafu ya kidijitali inaweza kusababisha kuyumba zaidi kwa uchumi kwa El Salvador na kuhimiza ufujaji wa pesa.


8. Mfilipino anatunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel kwa mara ya kwanza

Mwanahabari Maria Ressa alitunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel ya 2021 kwa kuripoti kwake kijasiri nchini Ufilipino juu ya mbinu tata za Rais Rodrigo Duterte katika vita dhidi ya dawa za kulevya. 

Yeye ndiye mshindi wa kwanza wa tuzo ya Nobel ya Ufilipino na alishinda tuzo hiyo pamoja na Dmitry Muratov wa Urusi, mhariri wa gazeti la Novaya Gazeta, ambalo linajulikana kwa ripoti yake muhimu kuhusu Kremlin.

Mwanahabari Maria Ressa alipata tuzo ya amani ya Nobel kwa ujasiri wake wa kutetea uhuru wa kujieleza. Picha| The Japan Times.

9. Ufaransa yawarudisha nyumbani mabalozi nchini Marekani kwa mara ya kwanza

Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza mnamo Septemba kuwa Marekani  itashirikiana na Australia katika uendeshaji wa teknolojia ya meli za kisasa ili kukabiliana na China katika eneo la Asia-Pasifiki. 

Muda mfupi kabla ya mpango huu kufanywa, Australia ilikataa makubaliano ya awali ya kununua manowari za kawaida kutoka Ufaransa. 

Ufaransa ambayo haikujulishwa kuhusu mpango huo, kwa hasira iliwaita mabalozi wake wanaoiwakilisha nchini Marekani kwa mara ya kwanza katika historia yake ndefu ya kidiplomasia na nchi hiyo iliyoanza mwaka 1778.


10. Kampuni ya vito duniani yatoa mkusanyiko wake wa kwanza wa almasi ulioundwa na maabara

Kampuni ya Pandora ya nchini Uingereza alitangaza kuacha kutumia almasi iliyochimbwa katika vito vyake na kuanzisha mawe yake ya kwanza ya syntetisk. 

Mkusanyiko wa Pandora Brilliance tayari umeanza nchini Uingereza na unatarajiwa kuingia katika masoko mengine mwaka wa 2022. Kampuni hiyo ilitaja uwezo wa kumudu na mahitaji ya wateja wa nyenzo zinazotokana na maadili na kuwajibika kwa mazingira kama sababu za mabadiliko hayo.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW