Zawadi za kielektroniki unazoweza kumpatia umpendae msimu wa sikukuu

December 18, 2020 5:02 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya zawadi hizo zimetikisa mwaka 2019 ikiwemo katika mtandao wa bidhaa za mtandaoni wa Amazon
  • Ni zawadi unazoweza kumpatia umpendae katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Dar es salaam. Msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka husubiriwa na watu wengi katika kipindi cha mwaka mzima. Msimu huo huwa ni muda maalum ambao watu hupata muda wa kupumzika, kutembeleana kama ndugu lakini vilevile ni muda maalum ambao watu hupata zawadi kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Zawadi hizo zinaweza kuwa mavazi, vifaa vya nyumbani au hata vifaa vya kielektroniki ambazo zimekuwa zikitazamiwa sana hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekuwa kwa kasi sana.

www.nukta.co.tz inaanza kwa kukuletea baadhi ya  zawadi za kielektroniki unazoweza kuwapatia ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kwa mujibu wa tovuti ya manunuzi mtandaoni Amazon,  vipo baadhi ya vifaa vya kielektroniki vilivyopo kwenye chati na orodha ya mapendekezo ya vitu vinavyoweza kuwa zawadi katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu. Sehemu kubwa ya vifaa hivi hupatikana katika maduka mbalimbali ya vifaa hivyo Tanzania. Zawadi hizo ni pamoja na;


1. Saa za kielektroniki (Smart Watch)

Hivi karibuni kampuni ya kimarekani ya Apple ilitoa matoleo mengi ya vifaa vya kielektroniki zikiwemo saa zenye uwezo mkubwa zaidi ya kusoma alama za nyakati. 

Saa hizo zina uwezo wa kupiga na kupokea simu, kutuma meseji vilevile zinaenda mbali na kuwa na uwezo wa kusoma mapigo ya moyo ya mtu pindi anapokuwa amevaa saa hiyo. Saa hiyo inaitwa Apple Series 5 inayouzwa dola 499 za kimarekani sawa na Sh 1.14 Milioni. Hupatikana katika maduka mbalimbali ya vifaa vya Apple nchini.

Zawadi inayoweza kudumisha furaha ya umpendae msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Picha | Mtandao.

2. Mashine kwa ajili ya unyooshaji mwili (Body Massager)

Mashine hizi zinajulikana kama “Body Massager” zinazoweza kusaidia pale mtu unanapokuwa na maumivu makali ya viungo vya mwili au baada ya kufanya kazi nzito siku nzima na kuwa na unahitaji wa kuunyoosha mwili. Mashine hii kwa mujibu wa Amazon inauzwa kwa gharama ya dola 108 sawa na wastani Sh248,000.


3. Kamera kwa matumizi ya ndani na nje. (Indoor/outdoor security camera)

Huenda kukawa na matukio mengi ya wizi na ujambazi katika kipindi hiki cha sikukuu watu wakiamini kuna vitu vingi vya thamani nyumbani, hivyo kwa kuwepo kwa vifaa kama kamera zinaweza kusaidia kujua matukio yote yanayoendelea ndani na nje ya nyumba na kuhakikisha kuna usalama wa hali ya juu. 

Gharama za kamera hizi ni kati ya dola 20-50 zinazohusisha kamera zenye uwezo wa kutumika bila waya (Wireless Cameras).

Kifaa hichi kinaweza kuwa zawadi nzuri kwa ndugu katika kumsaidia kwenye suala zima la usalama pindi anapokuwa nyumbani katika kipindi hiki ambacho huwa pia na huambatana na matukio ya kihalifu katika baadhi ya maeneo. 


Zinazohusiana:


4. iPhone 11 Pro 

Kama mfuko wako upo vizuri kumnunulia umpendaye ya simu janja aina ya iPhone 11 Pro yenye uwezo mkubwa zaidi ya simu nyingine zilizotengenezwa na Apple mwaka huu. Simu hiyo iliyotolewa rasmi mwezi Septemba imetikisa kwenye chati ya manunuzi katika mtandao huo wa Amazon. Gharama ya simu hiyo ni dola 999 sawa na Sh2.2 milioni.

Hayo ni mapendekezo ya baadhi ya bidhaa zilizotolewa na kampuni ya manunuzi ya bidhaa mtandaoni Amazon na zimetikisa sana katika chati ya manunuzi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Bidhaa hizo zinapatikana pia kwenye maduka mbalimbali ya vifaa vya kielektroniki nchini.

Simu ya kisasa ni zawadi nzuri ambayo inaweza kumfaa umpendae msimu huu wa sikukuu. Picha| Daniel Romero on Unsplash.

5. Smart Kitochi ni zawadi poa 

Kwa upande mwingine kuna zawadi nyingine nyingi zinazopatikana katika maduka mbalimbali hapa Tanzania unazoweza kumnunulia mpendwa wako kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka zikiwemo simu ndogo zinazotolewa na makampuni mbalimbali ya simu aina ya Smart Kitochi. 

Smart Kitochi ni simu ndogo yenye uwezo wa simu janja katika masuala ya mawasiliano. Ikiwemo uwezo wa kutumia programu tumishi ya Whatsapp na nyingine nyingi.


 6.  Kifaa cha upatikanaji wa intaneti nyumbani “Router”

Kifaa cha upatikanaji wa intaneti nyumbani “Router” inayoweza kutumika na watu hadi 6  yenye manufaa makubwa kwa watu nyumbani katika matumizi ya mtandao kwenye kipindi chote cha msimu wa sikukuu katika kuangalia Runinga au hata kutumia kompyuta na simu kwa ofa ya GB zinazotolewa baada ya kununua kifaa hicho.

Bidhaa hii inapatikana katika maduka mbalimbali nchini vilevile katika maduka ya mitandao mbalimbali ya simu kwa bei kati ya Sh75,000 mpaka Sh90,000

Zawadi hizi zinaweza kumwondolea upweke nduguyo anapokuwa nyumbani kwa kutumia kwa kutimiza mahitaji yake mbalimbali katika kipindi chote cha msimu wa sikukuu.

Enable Notifications OK No thanks