Majaliwa kuzindua uboreshaji wa daftari la kupiga kura Julai Mosi 2024

June 7, 2024 2:09 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Uboreshaji huo ni sehemu muhimu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2025.
  • Utafanyika kwa siku saba kuanzia Julai 1 hadi 7, 2024.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura utakaofanyika Julai Mosi mkoani Kigoma.

Jaji Jacobs Mwambegele ambaye ni mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) aliyekuwa akifungua mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 7, 2024 amesema baada ya kuzinduliwa kwa zoezi hilo vyama vya siasa vitaruhusiwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo. 

“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura, dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura…

…Kila chama kitaruhusiwa kuweka wakala mmoja kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa zoezi la uboreshaji kituoni ikiwemo kuwatambua wale wanaokuja kituoni kama wana sifa za kuandikishwa,” amesema Jaji Mwambegele.


Soma zaidi:Makamba: Safari za Rais Samia zina uhusiano na ustawi wa wananchi


Kuboresha daftari la kudumu la kupiga kura ni miongoni mwa matakwa ya kisheria nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwakani.

Jaji Mwambegele amesema kwamba mkutano huo uliofanyikaleo na vyama vya siasa ni sehemu ya utamaduni wa tume iliojiwekea wa kuwashirikisha wadau wa uchaguzi wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

Aliwataja wadau hao kuwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wawakilishi wa asasi za kiraia, wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, maafisa habari wa mikoa na halmashauri, wawakilishi wa makundi mbalimbali ya vijana, watu wenye ulemavu na wanawake.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K wa  mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam.Picha|INEC.

” Niwaombe viongozi wa vyama vya siasa kwa umoja wenu kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji na maelekezo ya tume kuhusu zoezi la uboreshaji wa daftari. Tume kwa upande wetu tutazingatia Katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi hili la uboreshaji,” ameongeza jaji Mwambegele..

Aidha, Mkurugenzi wa INEC Kailima, R. K amesema uboreshaji utafanyika kwenye mizunguko 13  ndani ya siku saba kuanzia Julai 1, hadi 7 mwaka huu katika vituo vyote vya kupiga kura nchini kama itakayobainishwa kwenye ratiba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV