Kwanini ni muhimu mwanamke wa Kiislam kukaa eda

September 10, 2026 6:03 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Baada ya kifo cha mumewe, anaruhusiwa kufanya majukumu yake huku akiendelea kuzingatia misingi ya dini yake.

Dar es Salaam. Siku tatu zilizopita Tanzania iliingia katika majonzi baada ya kumpoteza mume wa Rais Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir Hassan aliyefariki kwa ugonjwa wa moyo visiwani Zanzibar.

Baada ya kumalizika kwa shughuli ya kuanua matanga kwa mujibu wa dini ya Kiislamu kilichosalia ni kiongozi huyo wa nchi kukaa eda ambayo tayari ilishaanza tangu Septemba 7, 2026.

Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu eda ama iddah kwa Kiarabu ni muda ambao mwanamke anatakiwa kusubiri baada ya kuvunjika kwa ndoa kwa talaka au baada ya kufiwa na mume, kabla ya kuolewa na mwanaume mwingine. 

Kwa kawaida kipindi hiki huchukua kwa muda wa miezi minne na siku 10 ili kwa mjane, kuheshimu kipindi cha msiba wa mume, kutii sheria ya dini, kutoa muda wa kutafakari kuhusu ndoa pamoja na 

Swali linaendelea kugonga vichwa vya wengi ni Je, Rais Samia, kama mjane, anatakiwa kukaa eda? Na ni kwa namna gani anaweza kutekeleza majukumu yake ya kitaifa?

Eda haimaanishi kuacha majukumu

Kwa mujibu wa Sheikh Izzudini Alwy kutoka Kenya anasema Uislamu unatambua huzuni ya msiba, lakini haukusudii mwanamke kusimamisha maisha yake yote kwa sababu ya kifo.

“Siku tatu unafaa kuhuzunika. Lakini baada ya siku tatu lazima maisha yarudi katika hali ya kawaida.”

Sheikh Alwy anaeleza kuwa, eda yenyewe haimaanishi kuacha kila jukumu la lazima. Hivyo, suala la mwanamke kuendelea na kazi linapaswa kuangaliwa kwa kuzingatia aina ya kazi, umuhimu wake na masharti ya eda.

“Mwanamke aliyefiwa hakatazwi kutoka mchana, lakini usiku arudi kwake kulala nyumbani,” anasema Sheikh Alwy.

Akitoa mfano kutoka katika historia ya zama za Mtume Muhammad (S.A.W), Sheikh anaeleza kuhusu mwanamke aliyefiwa na mume wake akiwa na shamba ambalo lilihitaji kuendelea kuhudumiwa. Kwa mujibu wa maelezo yake, mwanamke huyo aliruhusiwa kuendelea na kazi hiyo.

Masharti mengine ya eda ni yapi?

Eda pia ina masharti yanayohusu namna mwanamke anavyojipamba na Sheikh Alwy anasisitiza kuwa kinachokatazwa si kuvaa nguo mpya, bali ni kujipamba kwa namna inayolenga kuonyesha uzuri.

“Kilichokatazwa si upya, kilichokatazwa ni pambo,” anasema.

Sheikh pia anataja hina, wanja, rangi za mdomo (lipstick), bangili, pete za kujipamba na manukato kuwa miongoni mwa mapambo anayopaswa kuyaepuka mwanamke aliye katika eda.

Masharti mengine ni kutokuruhusiwa kuolewa na mwanaume mwingine kabla eda haijaisha pamoja na kuficha ujauzito. 

Usikose makala ijayo ambapo tutaangazia aina za eda na tofauti zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
10 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
10 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
10 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mtihani darasa la saba kuanza kesho, 1,168,649 wakitarajiwa kuufanya

Mtihani darasa la saba kuanza kesho, 1,168,649 wakitarajiwa kuufanya

Nukta TV

Ajali yaua wanne Dar, watano wafariki mgodi wa dhahabu Gairo

Ajali yaua wanne Dar, watano wafariki mgodi wa dhahabu Gairo

Nukta TV

Mwanzo, mwisho sikia wasifu wa mume wa Rais Samia, Hafidh Ameir.

Mwanzo, mwisho sikia wasifu wa mume wa Rais Samia, Hafidh Ameir.

Nukta TV