Jiografia, historia kupewa kipaumbele vyuo vya Tanzania

January 28, 2021 11:34 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Masomo hayo yataanza kufundishwa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT).
  • Itawasaidia kuijua historia ya Tanzania kwa undani. 

Mwanza. Baada ya Rais John Magufuli kuagiza vyuo  kuanza kufundisha historia na Jiografia kuhusu Tanzania, hatimaye masomo hayo yataanza kufundishwa katika Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) katika mhula huu wa masomo ili kuwawezesha wanafunzi kuweza kujua mambo mengi ikiwemo  historia ya nchi yao.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha SAUT, Profesa Costa Ricky Mahalu amesema historia inaeleza kuwa licha ya vijana wengi kuhitimu vitivo mbalimbali vya elimu ya juu lakini wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusua historia yao na nchi yao.

Kutokana na changamoto hiyo, Professa Mahalu amesema wametenga kitengo maalum chuoni hapo kitakachoshughulika na suala hilo huku vijana wakipewa kibarua cha kuandaa makala inayohusiana na masomo hayo.

“Kiujumla somo la historia na jiografia halijapewa umuhimu mkubwa  na vijana wengi hawajui nchi na bara la Afrika lilipotoka na lilipo na hata mipaka ya nchi yao,” amesema Profesa Mahalu

Profesa Mahalu amesema wazo hilo la kufundisha masomo hayo vyuoni ni kutokana na wito wa Rais Magufuli kuwa wanafunzi waanze kufundishwa ili kuwaongezea vijana uelewa wa kutosha kuhusiana na nchi yao pamoja na rasilimali zake.


Zinazohusiana: 


Amesema maono ya Rais Magufuli yalilenga mbali na dhana yake ililenga kuona  nchi yake iliyopata uhuru miaka 56 iliyopita  inaendelezwa katika masuala ya  kisiasa na kiuchumi.

“Kwa  vijana wengi hawajui  historia ya Tanzania na  hawajui kwanini wazee na wahenga walianzisha vyama vya siasa  Afrika na Tanzania na kwamba kutokujua hayo yote  ni vigumu kujua kwanini Tanzania ilitawaliwa na ikaomba uhuru,” amesema. 

Msukumo wa kufundisha somo hilo utasaidia kutoa elimu kwa wanavyuo ili kuwa na uelewa wa namna watakavyoisaidia nchi katika masuala hayo.

“Tunapenda kuona vijana wanatumia maarifa wanayoyapata vyuoni katika kujiajiri, wawe wabunifu na si kutegemea ajira za Serikali na asasi za kiraia pekee,” amesema.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV