Masaju: Mafunzo ya Mujibu wa Sheria JKT yawe mwaka mmoja

November 28, 2025 5:19 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza  vijana kujitambua, kujenga maadili na kuongeza hamasa ya uzalendo.

Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Tanzania George Masaju amesema ipo haja ya Serikali kurejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yanayotolewa kwa mujibu wa sheria kuwa ya mwaka mmoja badala ya miezi mitatu inayotolewa hivi sasa.

Jaji Masaju aliyekuwa akizungumza leo Novemba 28, katika mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama mkoani Tanga amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza uzalendo kwa vijana wa Tanzania.

Aidha, Masaju ameongeza kuwa pamoja na uzalendo, vijana watajifunza stadi mbalimbali za maisha zitakazowawezesha kuwa wabunifu jambo litakalosaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira.

“Tumeshauri kuna uhumimu wa kuirejesha National Service (mafunzo) ambayo tutakaa kule mwaka mmoja. Akili yetu iwe nzuri, tujifunze skills (ujuzi)  za maisha za uzalishaji, kilimo, uvuvi, ufugaji, ufundi selemara na kila kitu tunachoweza kujifunza na kila fani,” amesema Jaji Masaju.

Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa kurejeshwa kwa mafunzo hayo kutatoa nafasi ya vijana si tu kupata mafunzo ya kijeshi, bali pia ujuzi wa uzalishaji, uajsiri, pamoja na kuimarisha udugu baina ya Watanzania kwa kuwa mafunzo ya JKT huwakutanisha vijana kutoka maeneo tofauti nchini.

“Wengine tulienda jeshini mwaka mmoja, miezi mitatu unajifunza mafunzo ya kijeshi, miezi tisa inayobaki ni uzalishaji. Moja ya faida tulipata kule ni ujasiri, tukajifunza uzalendo, tukaimarisha udugu wetu,” amesema Jaji Masaju.

Sambamba na hayo, amewasihi vijana kuwa na mwamko wa kulitambua na kulithamini Taifa, na kwamba upendo kwa nchi na watu wake ni nguzo muhimu ya amani na ustawi akisistiza kuwa iwapo Tanzania itaharibiwa kwa kukosa uzalendo hakutakuwa na nchi nyingine kwa kukimbilia.

JKT lilianzishwa rasmi Julai 10, 1963 kama chombo cha kitaifa kwa ajili ya malezi ya vijana, uzalendo, umoja wa kitaifa na huduma kwa Taifa na baada ya kuanzishwa rasmi, Bunge la Tanganyika lilipitisha sheria ya kuanzisha JKT ya mwaka 1964, iliyoweka misingi ya kisheria.

Awali, mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria yalitolewa kwa mwaka mmoja mpaka na kusitishwa mwaka 1994.

Hata hivyo, baada ya mafunzo hayo kurudishwa mwaka 2013, muda wa huduma kwa kundi la vijana wa mujibu wa sheria ilibadilishwa na kuwa miezi mitatu muda ambao ndiyo unatumika hadi sasa

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV