Jeshi la Magereza latangaza nafasi za ajira kwa vijana Tanzania

August 16, 2025 1:28 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ajira hizo ni kwa ajili ya vijana wakitanzania wenye elimu ya kidato cha nne  na ujuzi katika fani mbalimbali.
  • Wataogushi nyaraka watachuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Arusha. Jeshi la Magereza limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa kitanzania wenye elimu na ujuzi katika fani mbalimbali, likiwataka kutuma maombi yao kupitia mfumo wa ajira wa jeshi hilo kabla ya Agosti 29, 2025.

Taarifa ya Jeremia Katungu, Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo iliyotolewa Agosti 15, 2025 inabainisha kuwa  ajira hizo ni kwa ajili ya vijana wakitanzania wenye elimu ya kidato cha nne  na ujuzi katika fani mbalimbali kwa ngazi ya stashahada na shahada.

Miongoni mwa sifa zilizoanishwa na jeshi hilo ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania kuwa na kitambulisho cha uraia au namba ya utaifa kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Pamoja na sifa hiyo ya msingi taarifa ya Katungu imebainisha muombaji asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini, awe na umri kati ya miaka 18 hadi 24 kwa wahitimu wa kidato cha nne, na 18 hadi 28 kwa wenye ujuzi, pamoja na cheti cha kuzaliwa  na urefu usiopungua futi 5’4″ kwa wanawake na futi 5’7″ kwa wanaume.

“ (Muombaji) awe na siha na afya njema ya mwili na akili iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali, asiwe ameoa/kuolewa na asiwe amewahi kujifungua, asiwe na alama au michoro yoyote katika mwili wake (tattoo), awe na nidhamu na tabia njema na awe hajawahi kupatikana na hatia kwa shitaka la Jinai Mahakamani na hajawahi kufungwa.

… Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Askari Magereza na kufanya kazi mahali popote Tanzania bara, awe  tayari kujigharamia yeye binafsi katika hatua zote za awali za usaili wa ajira hii hadi kuripoti mafunzoni,” imesema taarifa ya  Katungu.

Aidha, Jeshi hilo limeanisha fani 15 za shahada na na moja ya stashahada zinazohitajika katika maombi ya nafasi hizo za ajira ikiwemo shahada ya uhandisi wa programu, sayansi katika teknolojia ya vyombo vya habari mseto na uhuishaji, usalama wa mifumo, uhandisi wa mitandao, saikolojia na ushauri nasaha na sayansi katika uhandisi wa uchimbaji madini.

Nyingine ni Stashahada ya Ufundi wa vifaa vya Ofisi,  Lugha za Alama, Uuguzi, Mitambo ya Kilimo, Mifugo,Kilimo.na Astashahada ya Katibu Muhtasi (Certificate in Secretarial).

Jinsi ya kutuma maombi

Jeshi la Magereza limesema maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Ajira wa Magereza (Tanzania Prisons Service Recruitment Management System (TPSRMS)) kwa kutumia kiunganishi cha  https://ajira.magereza.go.tz. na maombi yatakayotumwa kwa njia nyingine hayatapokelewa.

Pamoja na hayo Jeshi hilo limebainisha kuwa wombaji wote ambao walishafukuzwa katika kozi za mafunzo ya awali ya uaskari magereza hawaruhusiwi kuomba tena na wataogushi nyaraka watachuliwa hatua

“Mwombaji yeyote atakayewasilisha nyaraka za uongo/kughushi (Forged Documents) au kuficha sifa halisi ya elimu atakuwa ametenda kosa la jinai hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria,” imesema taarifa ya Katungu

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW