Apple waingiza sokoni simu mpya zinazotumia mfumo wa ‘eSIM’

September 14, 2018 7:07 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Simu hizo za iPhone ni mapinduzi ya teknlojia ya kisasa yasiyohitaji kadi tambulishi (SIM Card).
  • Watumiaji watawasiliano popote duniani bila kubadilisha simu au kuweka laini mpya.

Dar es Salaam. Umewahi kusafiri na simu yako ya iPhone ukalazimika kubadilisha laini ili kuendana na mtandao wa nchi husika au kutumia simu mbili kwasababu unahitaji kuwa hewani kwa namba mbili kama watumiaji wa simu za Android?

Basi jiandae kunufaika na simu mpya za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple kwasababu wamekuja na matoeo matatu ya iPhone XS, iPhone XS Max, na iPhone XR ambazo zinatumia laini zaidi ya moja bila kuwepo kwa line nyingine kwenye simu (eSIM).

Tofauti ya kutumia mfumo wa eSIM ni kwamba hautaweka laini mbili kama ilivyozoeleka katika simu za Android bali hii utaunganishwa moja kwa moja na mtandao unaotoa huduma ya simu.

Hata hivyo, matumizi ya  eSIM yataanza kutumika rasmi baada ya kuzinduliwa  mfumo wa iOS 12 kutoka mwishoni mwa mwaka huu ili kumuwezesha mteja kutumia mahali popote alipo.


Zinazohusiana: 


Kwa wateja ambao nchi zao hazina huduma ya eSIM watapelekewa simu za iPhone zenye uwezo wa kuingia line mbili ili kuwapa wateja uhuru wa kutumia simu moja.

Licha ya neema hiyo kwa wapenzi wa iPhone watalazimika kufunga mikanda kidogo ikizingatiwa kuwa gharama za simu hizo ni 1.7 milioni hadi 3.3 milioni kulingana na aina ya simu unayoitaka na uwezo wa kuhifadhi taarifa.

Ukiondoa bei umuhimu wa kununua simu hizo unabaki kutokana na sifa zake nyingine kama kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha, kukaa na chaji muda mrefu, kukaa kwenye kina cha maji cha futi 6.5 kwa dakika 30 pasipo kuharibika.

Watumiaji wa simu kutoka kampuni ya Apple wameonyesha mawazo tofauti kidogo kuhusu  mfumo wa eSIM na laini mbili kwa kuwa haujazoeleka kutumika katika simu za iPhone, lakini hawana jinsi zaidi ya kupokea mabadiliko hayo ya teknolojia.

“Mimi nimezoea yenye laini moja, hii ya mbele naweza kuhisi ni bandia,” amesema Emmanuel Feruzi ambaye ni mtumiaji wa simu za iPhone.

Hata hivyo, simu za iPhone Xs na iPhone Xs Max zinauzwa kwa oda maalum inayodumu kuanzia Septemba 14 hadi 21, 2018 ambapo bei hutegemea uwezo wa simu wa kuhifadhi vitu.  

Kwa upande wa iPhone Xs Max yenye uwezo wa 64GB itauzwa kwa Dola za Marekani 1,099, huku 256GB (Dola 1,249), na 512GB (Dola 1,449).

Kwako wewe mwenye shauku ya kununua simu yenye uwezo mkubwa kuliko zote tatu ya  iPhone XR inapaswa utasubiri kidogo hadi Oktoba 26 mwaka huu ambapo Apple kupokea oda kuanzia OKtba16,  2018.

 Aina za simu za iphone zinazotarajiwa kutumia mfumo wa eSIM  Picha| Phoneradar.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV