Waandishi Nukta Africa kuwania tuzo za Samia Kalamu 2025/26

September 3, 2026 5:48 pm · Shakrath Habibu
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na Daniel Samson na Esau Ng’umbi.
  • Dirisha la kupigwa limefunguliwa leo hadi Septemba 30, 2026.

Dar es Salaam. Wanahabari wawili kutoka kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa wamechomoza katika orodha ya wateule wa tuzo za Samia Kalamu zinazoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) pamoja na Bodi ya Ithibati (JAB).

Waandishi hao ni Daniel Samson ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mafunzo wa Nukta Africa na Esau Ng’umbi aliyewahi kuwa Mratibu wa Dawati la Habari wa kampuni hiyo.

Kazi za kihabari za waandishi wa Nukta Africa ni sehemu ya kazi 294 zilizopita katika chujio la majaji kati ya 3,003 zilizowasilishwa huku washindi wakitarajiwa kupatikana Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tuzo hizo, Peter Mwasalyanda aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Septemba 3, 2026 jijini Dar es Salaam amesema zoezi linalofuata ni kuzipigia kura kazi hizo.

“Kura za wananchi ni sehemu muhimu za mchakato wa kumpata mshindi, ushiriki wa wananchi katika hatua hii unatoa fursa adhimu kwa ajili ya kutoa mtazamo wao kuhusu thamani na umuhimu wa maudhui yaliyowasilishwa na waandishi wa habari na vyombo vya habari hapa nchini,” amesema Mwasalyanda.

Kwa mujibu wa Mwasalyanda, zoezi la upigaji kura limeanza leo na linatarajiwa kufungwa Septemba 30 mwaka huu, huku akiwataka wananchi kupiga kura kupitia tovuti rasmi ya www.samiaawards.tz  au kutuma ujumbe mfupi wenye neno “Ska” pamoja na namba ya mshiriki kwenda namba 15200.

Kwenye picha ya pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen akiwa na washindi wa tuzo kutoka Nukta Africa. Picha|Nukta Africa.

Hii ni mara ya pili kwa Nukta Africa kuingiza waandishi wake katika vinyang’anyiro vya tuzo nchini Tanzania ndani ya mwaka 2026.

Mei, 2026 wanahabari watatu kutoka Nukta Africa waliingia katika kinyang’anyiro cha tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) kwa mwaka 2024/25 zilizotolewa na MCT Mei 29 mwaka huu.

Katika kilele cha mashindano hayo Nukta Africa ilinyakua tuzo nne, tatu kutoka kwa waandishi Daniel Samson, Esau Ng’umbi na Kelvin Makwinya pamoja na tuzo maalum ya umahiri katika kuripoti masuala ya ugonjwa wa seli mundu (sicke cell).

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa wateule wa tuzo hizo, Daniel Samson amesema uteuzi huo unaonesha mchango wake katika tasnia ya habari na kugusa maisha ya watu kupitia makala na habari za kina zenye matokeo chanya kwenye jamii.

“Nimekuwa nikiandika habari za uchumi na biashara hasa kampuni changa (startups) na wajasiriamali kurasimisha biashara zao ili kulinda haki miliki zao. 

Kuteuliwa huku ni hamasa kwangu kuendelea kubobea zaidi katika uzalishaji wa maudhui bora yenye uchambuzi wa kina na yanayolenga kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida na kuchangia katika maendeleo ya Taifa,” amesema Samson.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV

Nukta Africa ndani ya Africa Agri Expo 2026

Nukta Africa ndani ya Africa Agri Expo 2026

Nukta TV