Bei ya mahindi yaibua mjadala bungeni, Spika aingilia kati

June 23, 2023 4:42 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yasema haijazuia watu kuuza nje ya nchi bali wafate taratibu.
  • Wafanyabiashara kutoka nje ya nchi watakiwa kusajili kampuni nchini.
  • Bashe atoa bei rasmi ya kununulia nafaka hiyo muhimu kwa chakula.

Dar es Salaam.Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali haijazuia wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi bali wafuate taratibu zilizowekwa huku akitangaza rasmi bei ya mahindi kuwa ni Sh800 kwa kilo katika makao makuu ya mikoa na Sh600 katika maeneo ya pembezoni.

Bashe aliyekuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Mbozi George Mwenisongole kuhusiana na zuio la kusafirisha mazao nje ya nchi amebainisha kuwa ni wafanyabiashara wa nje ya nchi pekee ndio wamezuiwa kuvusha mazao mipakani kwa kutumia madadali wa Tanzania.

Awali mbunge huyo wa Mbozi alimuomba Spika wa Bunge Tulia Ackson kujadili kwa dharula zuio la Serikali la kusafirisha mazao nje ya nchi jambo lililosababisha kuporomoka kwa bei ya mahindi na kufikia Sh7,000 kwa kilo 20 ambapo Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alitoa ufafanuzi.

“Tulichokataza kama Serikali ni mtu kutoka nje ya nchi kwenda shambani, kupakia mazao, kwenda mpakani na kumlipa dalali ili avushiwe mazao kwenda nje ya nchi…

…Tumekataza mfanyabiashara yoyote kufanya biashara ya mazao bila leseni ya biashara, bila kuwa na cheti cha mlipa kodi, bila kuwa na hati safi ya mlipa kodi, na bila kuwa na kibali cha kusafirisha mazao kwenda nje ya nchi,” amesema Bashe.

Aidha, kwa wafanyabiashara wa nje ili waweze kusafirisha mazao kwenda nje ya nchi wametakiwa kusajili kwanza kampuni zao hapa nchini kisha kufuata taratibu nyingine ambazo Serikali imeweka.

Bashe ameongeza kuwa wameweka taratibu hizo baada ya kubainika wafanyabiashara wengi kutoka nchini Tanzania wanapata changamoto ya mazao yao kuzuiwa na mamlaka za nchi nyingine wanapoenda kuuza kwa kuwa hawana vibali hivyo ambavyo ni muhimu na kukosekana kwa mapato yanayoendana na kiasi cha nafaka kilichoondoka nchini.

Itakumbukwa hivi karibuni malori zaidi ya 120 yenye shehena ya mahindi kutoka mikoa mbalimbali nchini yaliyokuwa yakisafiri kwenda nje ya nchi yalizuiliwa kwa siku nne eneo la Njiapanda ya Himo mkoani Kilimanjaro yasiendelee na safari baada ya kubainika kukosa vibali hitajika.

Sambamba na hilo Bashe ameongeza kuwa Serikali tayari imeshatoa bei elekezi ya kuuza nafaka ya mahindi ambayo ni Sh800 kwenye makao makuu ya wilaya na Sh600 kwenye maeneo ya pembezoni ambapo tayari Wakala wa Taifa wa Chakula NFRA Sh320 bilioni kwa ajili ya ununuzi wa mahindi ambapo tayari vituo vimeshafunguliwa.

Hata hivyo kutokana na baadhi ya wabunge kutokubaliana na ufafanuzi uliotolewa na Bashe Spika wa Bunge Tulia Ackson amewataka wabunge kuwaelekeza wananchi wao kuuza mazao kwenye vituo vya NFRA na kutoa taarifa ikiwa watabaini hoja ya Bashe haikuwa sahihi.

“Wabunge waambieni wananchi wenu wakauze mazao kwenye vituo vya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ( NFRA) kama wakikuta hakuna fedha ndio mje tujadili hapa kama hoja ya dharura,” amesema Tulia.

Hivi karibuni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa ziarani Mkoani Mwanza aliwaasa wakulima nchini kutouza mazao yao yote nje ya nchi katika msimu huu wa mavuno kwani huenda dunia ikakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na majanga yanayoikabili kwa sasa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na vita kati ya Urusi na Ukraine.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV