Waziri Bashe: Hamtakufa njaa

October 24, 2022 10:47 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema Serikali inapeleka mahindi maeneo yenye upungufu wa chakula.
  • Wananchi kuuziwa mahindi iliyo chini ya bei ya soko.
  • Kuanzisha kilimo cha umwagiliaji Kanda ya Ziwa. 

Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali imeanza kupeleka mahindi katika baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa na kuyauza kwa bei ya chini ili kuwanusuru wananchi na baa la njaa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya bei ya mahindi kuendelea kupanda nchini huku baadhi ya watu wakishindwa kumudu bei ya soko, jambo linalotishia uhai wa maisha yao. 

Sababu nyingine iliyochangia bei ya mahindi kupanda ni kufunguliwa kwa mipaka na kusuasua kwa mvua katika msimu wa mwaka huu na hivyo wakulima kupata mavuno kidogo. 

Hata hivyo, Waziri Bashe ameiambia Nukta Habari (www.nukta.co.tz) kuwa wananchi wa Kanda ya Ziwa wasiwe na hofu ya kufa njaa kwa sababu Serikali itawauzia mahindi kwa bei ya chini. 

Maeneo hayo ambayo yameanza kupokea mahindi ni pamoja na Wilaya za Ukerewe na Sengerema mkoani Mwanza , Bunda (Mara) na Mkoa wa Geita ambapo mahindi hayo yatauzwa kwa bei ya chini ya soko.

“Serikali ina akiba ya chakula cha kutosha hivyo wananchi hawatokufa njaa na kinachofanyika tunaangalia maeneo ambayo mahindi yamepanda sana na kupelekewa mahindi hayo yatakayouzwa kwa bei ya chini ya sokoni,” amesema Bashe.


Soma zaidi:   


Mipango ya muda mrefu kuwawezesha wakulima kuwa na akiba ya kutosha, amesema hivi sasa wataanzisha kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maji ya Ziwa Victoria ili kuwe na chakula kingi nchini.

Amesema kilimo hicho kitafanyika kwenye maeneo yote yaliyo karibu na Ziwa Victoria ikiwemo Mwanza kwa wilaya zote zilizopo kando kando ya ziwa, Mara na Kagera.

“Mungu katupa maji na tutaanza kuyatumia maji hayo na sasa tutaanza kujenga miundombinu ya umwagiliaji kuanzia Tarime mkoani Mara hadi Kagera lengo ni kutumia neema ya maji ambayo Mungu amatupatia,” amesema Bashe.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mapitio ya Uchumi ya Septemba 2022 (Monthly Economic Review) iliyotolewa na Benki ya Tanzania (BoT), gunia la kilo 100 la mahindi lilikuwa linauzwa kwa Sh89,039 Agosti mwaka huu.

Bei hiyo imepanda kutoka Sh44,811 iliyorekodiwa kipindi kama hicho mwaka jana.

BoT katika ripoti hiyo imeeleza kuwa akiba ya chakula katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ilikuwa tani 144,410 hadi kufikia Agosti 2022 ikiongezeka kutoka tani 140,695 zilizokuwepo mwezi uliotangulia.

Pia Agosti, NFRA iliza tani 2,009.2 za mahindi kwa wafanyabiashara na wakoboaji nafaka huku ikinunua tani 5,966.3 za mahindi na tani 211.5 za mtama.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV