Dola ya Marekani yaendelea kuimarika dhidi ya shilingi Tanzania
- Dola ya Marekeni yaendelea kuimarika kidogo katika soko la dunia pia.
Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeendelea kuonyesha nguvu dhidi ya shilingi ya Tanzania, huku viwango vya ubadilishaji fedha vya benki za CRDB na NMB leo Septemba 14, 2026.
Kwa mujibu wa viwango hivyo, CRDB inauza dola moja kwa Sh2,680, baada ya kuinunua kwa Sh2,600. NMB, kwa upande wake, inauza dola kwa Sh2,675 na kuinunua kwa Sh2,595.
Hali hiyo inaifanya dola kuendelea kuwa miongoni mwa sarafu zenye ushawishi mkubwa katika shughuli za biashara na miamala ya kimataifa inayohusisha Tanzania, ikiwemo malipo ya bidhaa na huduma zinazoagizwa kutoka nje.
Mbali na dola, Euro inanunuliwa kwa Sh2,917.97 na kuuzwa kwa Sh3,217.97 CRDB, wakati NMB inanunua kwa Sh2,894 na kuuza kwa Sh3,194.
Kwa pauni ya Uingereza, CRDB inanunua kwa Sh3,425.24 na kuuza kwa Sh3,725.24, huku NMB ikinunua kwa Sh3,363 na kuuza kwa Sh3,718.
Viwango vya ubadilishaji fedha hubadilika kulingana na mwenendo wa soko na sera za kifedha, hivyo bei za sarafu zinaweza kutofautiana kutoka benki moja hadi nyingine na kubadilika ndani ya siku.
