Mfumuko wa bei wafikia asilimia 4.2 Tanzania

June 9, 2026 4:00 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kiwango cha mfumko wa bei cha Mei 2026 ndio kiwango cha juu zaidi kwa miaka mitatu iliyopita.
  • Kenya imeongoza kwa kurekodi asilimia 6.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.1 ikilinganishwa na mwezi uliopita.

Arusha. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini  Tanzania kwa mwezi Mei, 2026 umefikia asilimia 4.2 kutoka asilimia 4 kwa mwaka ulioishia mwezi April, 2026 ikichangiwa zaidi na kupaa kwa mfumuko wa bei wa huduma za usafiri.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2026 imeongezeka kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi uliopita.

Taarifa ya mwenendo wa mfumuko wa bei nchini iliyotolewa Juni 8, 2026 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imebainisha kuwa kiwango hicho cha mfumuko wa bei ni imara.

“Fahirisi za Bei zimekuwa na mwenendo imara kutoka mwezi Mei, 2025 hadi mwezi Mei, 2026 ikipishana kidogo katika kiwango cha 119.85 na 124.90 mtawalia. Katika kipindi hicho, Mfumuko wa bei pia umekuwa na mwenendo imara kati ya asilimia 3.2 na asilimia 4.2,” imesema taarifa ya NBS.

Kiwango cha mfumko wa bei cha Mei 2026 ndio kiwango cha juu zaidi kwa miaka mitatu iliyopita. .

Kiwango cha juu zaidi cha mfumuko wa bei kilichorekodiwa katika kipindi hicho kilikuwa asilimia 4 Mei 2023. Katika miezi iliyofuata, kiwango hicho kiliendelea kupanda na kushuka, kikibadilika ndani ya wastani wa kati ya asilimia 3 na asilimia 3.9. 

Licha ya mfumuko huo kupaa, bado kiwango hicho kipo ndani ya wigo wa Serikali wa kuwa na mfumuko wa bei kati ya asilimia 3.0 na asilimia 5.0.  

Mchambuzi wa masuala ya uchumi na fedha Paulo Chengula aliambia Nukta Habari kuwa ili kupunguza maumivu ya kupaa kwa mfumuko huo wa bei wananchi wanapaswa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuandaa mfumo mzuri wa bajeti binafsi kuendana na kipato.

“Mwananchi anatakiwa sasa ajiandae na awe na bajeti, aache baadhi ya matumizi ambayo sio ya muhimu,” amesema. 

Kenya kinara EAC

Wakati mfumuko wa bei nchini Tanzania ukionyesha mabadiliko kidogo, nchi jirani ya Kenya imeongoza kwa kurekodi asilimia 6.7, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.1 ikilinganishwa na mwezi uliopita, huku Uganda ikiwa na kiwango cha chini zaidi cha asilimia 3.2 miongoni mwa nchi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Sin

Nukta TV

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Mizinga ya heshima, Rais Samia akimpokea Rais wa Singapore, Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV