Wagonjwa wa Corona wazidi kuongezeka Tanzania

March 19, 2020 8:58 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Wizara ya Afya yathibitisha wagonjwa wengine wawili wa Corona leo na kufanya jumla ya wagonjwa kuwa sita mpaka sasa.
  • Wagonjwa wote wawili ni Watanzania walioingia nchini kwa nyakati tofauti. 
  • Serikali yawataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amethibitisha kuongezeka kwa visa vingine viwili vya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania na kufanya jumla ya wagonjwa kufikia sita. 

Taarifa iliyotolewa na Waziri huyo leo (Machi19, 2020), hadi sasa Tanzania ina wagonjwa sita ambapo watano wanatokea Tanzania bara na mmoja anatokea Zanzibar kama ilivyoripotiwa jana Machi 17, 2020. 

“Wagonjwa wapya wawili wamethibitika jijini Dar es salaam kuwa na Covid-19, na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa waliothibitika nchini mpaka sasa kufikia 06 (sita), ambapo mmoja ni yule wa Zanzibar aliyetolewa taarifa jana,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo, Ummy amesema wagonjwa wote wawili ni Watanzania, wanaume wenye umri wa miaka 40 kila mmoja.

Mmoja alisafiri nchi za uswisi, Denmark na Ufaransa kati ya Machi 5, 2020 hadi Machi 13 na kurejea nchini Machi 14.

Mwingine alisafiri kwenda Afrika Kusini kati ya Machi14, 2020 hadi Machi 16 na kurudi nchini usiku wa Machi 17.

Wagonjwa hao wametengwa na juhudi za kuendelea kuwafuatilia watu waliokuwa nao karibu zinaendelea.

“Wahusika wote wametengwa (isolation) na hali zao zinaendelea vizuri. Juhudi za kufuatilia watu waliokuwa karibu na wagonjwa waliothibitika kuwa na COVID-19 (yaani “contacts”) zinaendelea,” amesema Ummy.

Aidha, amebainisha kuwa hadi sasa jumla ya watu 46 wanafuatiliwa jijini Arusha, na watu 66 wanafuatiliwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mara ya kwanza, Tanzania ilithibitisha mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo  Machi 16, na visa vitatu viliongezeka jana huku kimoja kikiripotiwa Zanzibar.


Zinazohusiana


Mpaka sasa ni nchi tatu za Afrika Mashariki; Tanzania, Kenya na Rwanda ndiyo zimethibitisha kuwa na wagonjwa wa virusi vya Corona, ambapo  jana Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema barani Afrika kuna kesi 233 za watu walioambukizwa. 

Wananchi wameshauriwa kuwa watulivu na kuchukua tahadhari zinazotolewa na mamlaka za afya nchini ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kugusa mdomo, pua na macho. 

Pia kutumia tishu wakati wa kukohoa na kuepuka mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV