Kimbunga Jobo kutua Dar, mikoa mengine kuathirika

April 23, 2021 11:55 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mikoa hiyo ni Mtwara, Lindi, Tanga, Mafia, Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.
  • Kinatarajiwa kuleta athari za upepo mkali, mawimbi makubwa baharini na mvua kubwa.
  • Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari ikiwemo kusitisha kwa muda shughuli za baharini. 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kuwa kimbunga Jobo kinachozidi kusogea ukanda wa Pwani wa Tanzania kinatarajiwa kutua Dar es Salaam Aprili 25 huku kikitarajiwa kuleta athari za upepo mkali, mawimbi makubwa baharini na mvua kubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk Agness Kijazi amewaambia wanahabari jijini Dar es Salaam kuwa kimbunga kama hicho hakijawahi kutokea tangu mwaka 1952 na kuwasihi Watanzania hasa wanaofanya shughuli zao baharini kuchukua tahadhari zikiwemo kusitisha shughuli zao kwa muda kutazamia mwelekeo wake.

 “Kimbunga kitakachotua Dar es Salaam kitakuwa kimepungua nguvu kitakuwa na kilomota 60 kwa saa. Lakini tufahamu kuwa kasi ya kilomita 60 kwa saa japo kuwa ni nguvu iliyopungua ikilinganishwa na jinsi upepo ulivyo sasa bado ni mkubwa unaweza kuleta athari,” amesema Dk Kijazi.

Amewataka wakazi wa mikoa ya ukanda wote wa Pwani kuanzia Mtwara, Lindi, Tanga, Mafia, Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar kuchukua tahadhari ya upepo mkali unaotarajiwa wa kimbunga kitakachokuwa Jumapili hii.

Dk Kijazi amewasihi wanaotumia bahari hususan wavuvi na wengineo kuchukua tahadhari ikiwemo kusubiri kwanza kutazamia mwenendo wa kimbunga hicho.

“Kwa sasa hivi wananchi wachukue tahadahari wale wanaotumia bahari ambako kimbunga hiki kipo kuna upepo mkali baharini pamoja na mawimbi makubwa. Mtu aangalie chombo chake katika usawa baharini kama kinaweza kustahimiri.

“Kwa wavuvi katika ukanda wa Pwani ni bora wakasubiri kwanza hali ya kimbunga kiweze kupita weweze kuendelea sasa na shughuli zao,” amesema.


Soma zaidi:


Dk Kijazi amesema kuwa mamlaka mbalimbali za Serikali zitatoa matamko kwa wananchi juu ya  hatua ya kuzitekeleza na maeneo ambayo shughuli zinaweza kusitishwa.

Mbali na ukanda wa Pwani, Dk Kijazi amesema kimbunga hicho kinaweza kuathiri hadi ukanda wa Magharibi kwa kuleta mvua kubwa.

“Vimbunga kama hivi si kawaida kutokea katika maeneo yaliyo karibu na Ikweta. Tuna muda mrefu haikijawahi kutokea. Mwaka 1872 kulikuwa na kimbunga kilitua Dar es Salaam. Lakini 1952 kilikuwepo kimbunga Lindi kiliweza kuleta athari. 

TMA imewataka wananchi kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka TMA pamoja  na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Nukta TV

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Nukta TV

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Nukta TV