TMA: Kimbunga ‘Freddy’ hakina madhara kwa sasa

February 20, 2023 10:03 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yasema sehemu zote za nchi zipo salama
  • Wananchi watakiwa kuzingatia taarifa na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ufafanuzi kuhusu uwepo wa  kimbunga ‘Freddy’ kilichopo kusini magharibi mwa bahari ya Hindi karibu na pwani ya Madagascar, kilichotarajiwa kuikumba pwani ya afrika mashariki mwanzoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa ufafanuzi huo uliotolewa leo February 20,2023, TMA imesema kimbunga hicho hakina madhara ya moja kwa moja  kwenye maeneno mengi yaliyopo nchini tofauti na upotoshaji unaoendelea kwenye kwenye mitandao ya kijamii.

“TMA inaendelea kufuatilia kwa kina mwenendo wa kimbunga hiki na itatoa taarifa punde tu kutakapokuwa na haja ya kufanya hivyo”, inasema taarifa hiyo.

Kwa takribani  kipindi  cha wiki moja iliyopita kulizuka taarifa ya ujio wa kimbunga hicho ikiripotiwa na vyombo vya habari mbalimbali vya kitaifa na mamlaka za hali ya hewa za kimataifa ikiwemo Taasisi ya Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Hii si mara ya kwanza kwa tahadhari za vimbunga kutangazwa ukanda wa Afrika Mashariki na nchini Tanzania,.

 Mwaka 2021 mamlaka hiyo ilitangaza ujio wa kimbunga ‘Jobo’   kilichotarajiwa kuathiri maeneo ya pwani ya Tanzania mnamo April 25,2 2021.

Kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa upepo kinzani kwenye ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kimbunga hicho kilizidiwa nguvu na kushindwa kuathiri maeneo yalyliyokusudiwa.


Soma zaidi


Wananchi zingatieni taarifa za tahadhari

Kupitia taarifa hiyo TMA imewata ka wananchi  na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalamu katika sekta husika ili kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.

Pamoja na hayo imewakumbusha wananchi wanaojihusisha na kusambaza taarifa zisizo na ukweli kuhusu hali ya hewa nchini kuacha mara moja kwani ni kinyumme na sheria na taratibu.

“Mamlaka inapenda kuikumbusha jamii na umma kwa ujumla kuwa kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya 2019, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutoa taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa na ni kosa kisheria mtu mwingine kufanya hivyo,” imesema TMA .

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV