Chanjo ya Uviko-19 haisababishi ugonjwa wa kupooza
- Hakuna uthibitisho wowote unaoonyesha chanjo ya Uviko-19 inasababisha ugonjwa wa kupooza.
- Inashauriwa mtu kupata ushauri wa daktari kabla ya kupata chanjo.
Dar es Salaam. Kumekuwa na uvumi mwingi mara baada ya chanjo ya Uviko-19 kuanza kutolewa katika nchi mbalimbali duniani. Moja ya uzushi ni kuwa chanjo hiyo husababisha ugonjwa wa kupooza kwa watoto na watu wazima.
Hakuna uthibitisho wowote wa kitaalamu unaoonyesha uhusiano kati ya chanjo ya Uviko-19 na ugonjwa wa kupooza katika mwili wa binadamu mara baada ya kupata chanjo.
Pia wataalam wa afya hawajaripoti kesi za watu kupooza baada ya watu kupatiwa chanjo.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu anaweza kupata changamoto ndogo ndogo mara baada ya kupata chanjo.
Ndiyo maana inashauriwa mtu kukaa katika kituo cha afya alipopatia chanjo kwa dakika 15-30 ili kuangalia mabadiliko yatakayotokea katika mwili wake mara baada ya kupata chanjo.
Vilevile inashauriwa kupata ushauri wa daktari kabla ya kupata chanjo ili kujua namna inavyoweza kufanya kazi kulingana na mwili wako.
Hivyo, kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanaamini chanjo inasababisha kupooza, fahamu kuwa huo ni uzushi na unashauriwa kwenda kupata chanjo ya Uviko-19 katika eneo lako ili uwe salama.
Latest