Chanjo ya Uviko-19 haisababishi kansa

October 15, 2022 8:37 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Chanjo ya Uviko-19 haichanganyiki na vinasaba vya mtu ili kusababisha kansa.
  • Chanjo zote za Uviko-19 zimehakikiwa na kufanyiwa majaribio kabla ya kutolewa.

Dar es Salaam. Wakati harakati za kuhamasisha chanjo ya Uviko-19 zikiendelea duniani, kumezuka uzushi kuwa chanjo ya ugonjwa huo inasababisha kansa, jambo ambalo si kweli.

Taarifa hiyo ya uzushi inayosambaa kwa njia ya video kupitia mtandao wa Twitter imezitaja aina za chanjo ambazo zinadaiwa kuwa na viambata vya sumu vinavyosababisha ugonjwa wa kansa.

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa 31 Machi, 2022 inasema chanjo zote ni salama, kabla ya chanjo kutolewa hupitia michakato mbalimbali ikiwemo upimaji na majaribio.

“Chanjo za Uviko-19 zimejaribiwa katika majaribio makubwa yaliyodhibitiwa ambayo yanajumuisha watu wa maeneo mbalimbali, jinsia zote, makabila tofauti na wale walio na hali za kiafya zinazojulikana,” inasema taarifa ya WHO.

Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa (CDC) kwenye taarifa yake iliyotolewa Septemba 12, 2022 kinaeleza kuwa chanjo ya Uviko-19 inaupa mwili kinga dhidi ya virusi na hakuna chanjo inayosababisha mtu kupata kansa.


Soma zaidi


Nini husababisha kansa?

Kwa mujibu wa kituo hicho, ili mtu apate ugonjwa wa kansa ni lazima virusi hivyo vichanganyike na vinasaba vya muhusika, lakini chanjo za Uviko-19 haziingii kwenye mfumo wa seli za nyuklia  zilizopo mwilini ambapo vinasaba huwepo.

Hivyo madai ya kuwa chanjo ya Corona kusababisha kansa si ya kweli.Nini  husababisha kansa?Kwa mujibu wa WHO ugonjwa wa kansa unasababishwa na matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe, lishe duni,na sababu nyingine za maambukizi ya magonjwa yasiyoambukiza

Kansa pia husababishwa na virusi aina mbalimbali kama “Helicobacter pylori, human papillomavirus (HPV), Epstein-Barr virus (2)”,virusi vya hepatitis B na C.

Virusi hivyo  vinavyosababisha maambukizi hueneza DNA zao, na kuathiri muundo wa maumbile wa seli zenye afya na uwezekano wa kuzifanya zigeuke kuwa saratani.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW