Hapana: Chanjo ya Corona haivurugi mzunguko wa hedhi kwa wanawake

August 26, 2021 11:26 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya wazushi kuwatisha wanawake wasipate chanjo.
  • Wanawake waliopata chanjo wasema mizunguko yao ya hedhi haijaathirika.
  • Mpaka sasa hakuna ripoti zilizotolewa na wataalam kuhusu athari za chanjo kwa wanawake.

Dar es Salaam. Habari za uzushi kuhusu chanjo ya Uviko-19 zinaendelea kusambaa kwa kasi mtandaoni na safari hii wapotoshaji wamehusisha chanjo hiyo na kuvuruga mzunguko wa hedhi kwa wanawake, jambo ambalo siyo la kweli.

Katika mitandao ya kijamii, baadhi ya watu wanawatisha wanawake kuwa wasipate chanjo ya Uviko-19 wakidai kuwa inaathiri mwenendo wa hedhi ikiwemo kuzidisha siku za hedhi.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi ambao umetolewa kuhusu dhana hiyo. 

Baadhi ya wanawake ambao wamepata chanjo hiyo nchini Tanzania walioongea na Nukta Habari (www.nukta.co.tz) wamesema tangu wachanjwe hawajaona mabadiliko yoyote kwenye miili yao.

Mkazi wa Kigoma, Jackline Thomas aliyepata chanjo wiki kadhaa zilizopita amesema mzunguko wake wa hedhi uko kawaida na hajapata mabadiliko yoyote tangu achanjwe.

“Nimeingia period (hedhi) kawaida tu kama ninavyoingiaga sijapata tofauti yoyote baada ya kwenda kuchanja,” amesema Jackline.

Naye Nsajigwa Gerald kutoka mkoani Mbeya amesema alichelewa siku moja kupata hedhi ila haimpi kuamini kuwa mabadiliko hayo yamesababishwa na yeye kuchanjwa chanjo ya Uviko-19.

“Nimezoea kujihesabia siku. Safari hii nilichelewa siku moja ila siku zangu hazikuzidi kama wanavyosema,” amesema Nsajigwa.

Mpaka sasa hakuna ripoti zilizotolewa na wataalam kuhusu athari za chanjo kwa wanawake. Picha | Fierce Healthcare.

Baadhi ya wanawake ambao wamepata chanjo hiyo nchini Tanzania walioongea na Nukta Habari (www.nukta.co.tz) wamesema tangu wachanjwe hawajaona mabadiliko yoyote kwenye miili yao.

Mkazi wa Kigoma, Jackline Thomas aliyepata chanjo wiki kadhaa zilizopita amesema mzunguko wake wa hedhi uko kawaida na hajapata mabadiliko yoyote tangu achanjwe.

“Nimeingia period (hedhi) kawaida tu kama ninavyoingiaga sijapata tofauti yoyote baada ya kwenda kuchanja,” amesema Jackline.

Naye Nsajigwa Gerald kutoka mkoani Mbeya amesema alichelewa siku moja kupata hedhi ila haimpi kuamini kuwa mabadiliko hayo yamesababishwa na yeye kuchanjwa chanjo ya Uviko-19.

“Nimezoea kujihesabia siku. Safari hii nilichelewa siku moja ila siku zangu hazikuzidi kama wanavyosema,” amesema Nsajigwa.

Wataalamu wanasemaje? 

Wataalam wa afya likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) mpaka sasa hawajaripoti kesi za wanawake waliochanjwa chanjo kupata changamoto za uzazi ikiwemo kuvurugika kwa hedhi.

Dk Frank Msafiri kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (Muhas) amesema taarifa hizo si za kweli kwani katika takwimu walizonazo za wanawake wote waliopata chanjo hakuna ambaye amepata tatizo la kuzidisha mzunguko mara baada ya kupata chanjo hiyo.

Hivyo hakuna uhusiano wowote kati ya chanjo na siku za hedhi za mwanamke.

“Katika wanawake wote wanaotumia chanjo, hamna ambaye chanjo imeathiri mzunguko wake wa hedhi au uwezo wake wa kushika mimba,”amesema Dk Msafiri wakati akiongea na Nukta Habari.

Amesema inashauriwa mtu anapopata madhara yoyote makubwa baada ya kupata chanjo apate ushauri wa daktari ili kuona kama kuna tatizo lingine tofauti na chanjo.

Wananchi wanahimizwa kwenda kuchanjwa ili wajiweke salama dhidi ya Uviko-19 na kuwakinga wengine.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW