Upungufu wa vyoo bado kitendawili Pangani

February 15, 2022 8:19 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Uwiano wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi katika shule za msingi upo juu ya uwiano wa Kitaifa.
  • Hali hiyo inawaweka wanafunzi hao hatarini kupata magonjwa ya mlipuko.

Dar es Salaam. Ripoti ya TakwImu Muhimu za Elimu 2020 (BEST 2020) zilizotolewa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) iinaonesha kuwa uwiano wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi katika shule za msingi wilayani Pangani, mkoani Tanga upo juu zaidi ya uwiano wa Kitaifa, jambo linalowaweka hatarini wanafunzi hao.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, tundu moja la choo linatumiwa na wanafunzi 38 kwa upande wa wavulana,ikiwa ni juu ya uwiano wa Kitaifa wa tundu moja kwa wavulana 25.

Kwa upande wa wasichana tundu moja la choo linatumiwa na wanafunzi 35, tofauti na uwiano wa Kitaifa wa tundu moja kwa wasichana 20.

Hali hiyo inawaweka hatarini wanafunzi kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na kuhara, ambayo yanaweza sababisha wanafunzi hao kutokuhudhuria darasani na kufanya vibaya kwenye masomo yao.

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV