Tanzania mwenyeji mkutano wa kimataifa wa utalii

May 20, 2022 9:24 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mkutano wa kimtaifa utalii wa Shirika la Utalii Dunia (UNWTO).
  • Utafanyika Arusha Oktoba mwaka huu.
  • Utajadili namna ya kuimarisha sekta ya utalii Afrika.

Dar es Salaam. Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimtaifa utalii wa Shirika la Utalii Dunia (UNWTO) Kamisheni ya Afrika ambao unalenga kujadili za namna ya kuiimarisha sekta ya utalii Afrika ili kuhimili majanga mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona (Uviko-19).

Mkutano huo utakaofanyika jijini Arusha Oktoba 5 hadi 7, 2022 unatarajiwa kuhudhuriwa na mawaziri wa utalii a uhifadhi wanachama wa UNWTO na kufuatiwa na jukwaa la wazi kujadili kwa kina na kutoka na mapendekezo ya namna ya kujenga upya ustahimilivu wa utalii wa Afrika kwa maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi.

Huenda mapendekezo hayo yakasaidia kuimarisha sekta ya utalii Afrika kwa kuongeza idadi ya watalii na mapato baada ya Uviko-19, igonjwa ambao uliwafanya watu wengi kukosa kazi na kupungua kwa uhifadhi wa maliasili na bidhaa zinazotumika katika utalii.

Ili kufanikisha mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Francis Michael amezinduwa rasmi kamati ya kitaifa ya maandalizi ya mkutano huo wa 65 (65th UNWTO-CAF MEETING).

“Nategemea kamati hii itafanya kazi kwa weredi, maarifa na kuwa na kasi kubwa katika maandalizi haya,” amesema Dk Michael.

Amesema yupo tayari kushirikiana na kamati hiyo ili Tanzania iwe mfano kwa nchi nyingine wananchama wa umoja huu.  

“Nina nafasi ya kufanya mabadiliko ya wajumbe wakati wowote pale ninapoona maandalizi yanalegalega”, amesema Dk Michael Mei 19, 2022 wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Arusha. 


Zinazohusiana:


Kamati hiyo itakuwa na wenyeviti wenza wawili ambao ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Felix John na mwenyekiti mwenza, Rahim Bhaloo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT).

Wenyeviti hao wataongoza kamati ya wajumbe kutoka kwenye baadhi ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, taasisi na idara za wizara mbalimbali, vyama vya wadau wa utalii na waandishi habari wa Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa TTB, Felix John amesema, “Mkutano wa 65 wa UNWTO kufanyika Tanzania ni sehemu ya utekelezaji wa vitendo wa mkakati wa Bodi ya Utalii wa kutangaza na kukuza utalii wa mikutano ambao unalenga kuvutia mikutano mingi ya kimataifa kufanyika nchini Tanzania.”

Amewataa wadau wa utalii  wajitayarishe kutoa huduma nzuri kwa wageni ili tuendelee kuiweka nchi ya Tanzania kwenye nafasi nzuri ya kuaminiwa kuandaa mikutano mingine ya kimataifa.

Mwenyekiti ZCT, Rahim Bhaloo ameeleza kuwa mkutano huo ni fursa kwa nchi ya Tanzania kuuza mazao ya utalii na uwekezaji katika sekta ya utalii. 

Vilevile ni fursa kwa mwananchi kuwa wabunifu ili waweze kufanya biashara na kujiongezea kipatao kupitia mkutano huo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV