TMA yataja sababu ongezeko la joto baadhi ya mikoa Tanzania

November 17, 2022 12:34 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni upungufu wa mvua na kusogea kwa jua la utosi.
  • Joto kuendelea hadi mwishoni mwa Novemba.
  • Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari. 

Dar es Salaam. Kufuatia kuripotiwa kuongezeka kwa joto katika baada ya mikoa nchini Tanzania ikiwemo Dar es Salaam, watalaam wa hali ya hewa wameeleza kuwa hali hiyo inashababishwa na kusogea kwa jua la utosi na upungufu wa mvua.

Oktoba mwaka huu, hali ya joto iliongezeka katika maeneo mbalimbali nchini. Kiwango cha juu zaidi cha joto cha nyuzi joto 36.9 kiliripotiwa Mpanda, Katavi Oktoba 26, 2022. 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kiwango hicho ni sawa na ongezeko la nyuzi joto 4  ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Oktoba. 

Baadhi ya maeneo mengine yaliyokuwa na ongezeko la joto Oktoba ni pamoja na Mkoa wa Tabora nyuzi joto 35.7 (ongezeko la nyuzi joto 3.0), Mji wa Moshi nyuzi joto 34.1 (ongezeko la nyuzi joto 3.2) na Dar es Salaam nyuzi joto 32.8 (ongezeko la nyuzi joto 1.4).

TMA katika taarifa yake iliyotolewa leo Novemba 17, 2022 imesema katika wiki mbili za za Novemba, 2022, hali ya ongezeko la joto iliendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo ambapo kituo cha Mpanda kiliripoti nyuzi joto 35.4 Novemba 2, 2022 ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 4.7 ukilinganisha na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Novemba. 

Kituo cha Tabora kiliripoti nyuzi joto 34.8 (ongezeko la nyuzi joto 3.7), Dar es Salaam nyuzi joto 33.7 (ongezeko la nyuzi joto 2.1) pamoja na Kilimanjaro nyuzi joto 34.3 sawa na ongezeko la nyuzi joto 2.4.

Wataalam wa afya wanashauri kunywa maji mengi kwa kuwa msimu huu humfanya mtu kupoteza maji mengi mwilini. Picha| Folio.

Sababu joto kuongezeka

“Hali hii imesababishwa na kusogea kwa jua la utosi sambamba na upungufu wa mvua katika maeneo mengi hapa nchini kama ilivyotabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania,” imeeleza TMA. 

Kwa kawaida vipindi vya jua la utosi nchini hufikia kilele mwishoni mwa Novemba wakati jua hilo likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa). 

Jua la utosi huambatana na hali ya ongezeko la joto kwa sababu uso wa dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na jua kuliko maeneo mengine.

TMA imeeleza kuwa vipindi vya ongezeko la joto vinatarajiwa kuendelea kujitokeza Novemba, 2022 hususan katika maeneo yanayotarajiwa kuendelea kuwa na upungufu wa mvua na kupungua kidogo ifikapo Disemba, 2022 ambapo ongezeko la mtawanyiko wa mvua unatarajiwa.

Mamlaka hiyo imewataka wananchi kufuatilia taarifa za mwenendo wa hali ya hewa zinazotolewa pamoja na kutafuta, kupata na kutumia ushauri wa wataalamu wa kisekta ili kuepuka au kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na hali mbaya ya hewa ikiwemo ongezeko la joto.


Soma Zaidi:


Ufanye nini kukabiliana na joto kali?

Unashauriwa kuvaa nguo zinazoendena na msimu wa joto ambazo ni nyepesi zenye uwezo wa kupitisha hewa katika mwili wako. Pia epuka kuvaa nguo zinasharabu mwanga wa jua zikiwemo nyeusi na hivyo kumuongezea mtu joto mwilini.  

Hakika unahitaji kuusikia upepo unapovuma na huwezi kuipata hisia hiyo kama umevaa nguo za kubana.

Ukivaa nguo za kukuachia kidogo, itakupunguzia adha ya kuonekana umeloa pale jasho linapotoka katika mwili wako.

Njia nyingine ni kunywa maji mengi kadiri inavyowezekana ili kufidia maji ambayo mwili wako unayapoteza kwa jasho na hata haja ndogo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
9 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
9 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Nukta TV

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV