Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

July 7, 2026 1:31 pm · Waandishi Wetu
Share
Tweet
Copy Link
  • Sehemu kubwa ya barabara jijini Dar es Salaam zina msongamano mdogo huku ulinzi ukiimarishwa kwenye makutano ya barabara kuu. 

Dar es Salaam. Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameshuhudia ulinzi mkali katika sehemu kubwa ya makazi yao wakati Watanzania wakiendelea kuadhimisha Sikukuu ya Sabasaba licha ya uwepo wa mpango wa maandamano. 

Baadhi ya watu mitandaoni wamekuwa wakihamasisha maandamano siku ya Sabasaba wakitaka Serikali ifanye maboresho ya kidemokrasia ikiwemo katiba mpya, kumaliza utekaji na kumwachia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lissu. 

Wanahabari wa Nukta TV na Nukta Habari wameshuhudia askari wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa doria katika sehemu kuu za makutano ya barabara na karibu na miundombinu ya umma. 

Sehemu kubwa ya maduka yakiwemo ya Manzese, Magomeni, Banana, Kinondoni, Kimara, Makumbusho, Mbezi Beach, Mwenge na Mabibo yalikuwa hayajafunguliwa hadi majira ya saa 4 asubuhi huku manyunyu yakinyesha katika baadhi ya maeneo.

Hali ilivyokuwa katika eneno la stendi ya mabasi ya Makumbusho jijini Dar es Salaam. Picha | Nukta Habari

Si kawaida kwa maeneo haya kushuhudia wafanyabiashara wakichelewa kufungua biashara zao katika siku nyingine za sikukuu au mwisho wa juma. Katika siku za sikukuu kama Sabasaba watumishi wengi wa umma na sekta binafsi huwa katika mapumziko. 

Hata hivyo, sehemu kubwa ya wafanyabiashara huwa wanaendelea na shughuli zao kama ilivyo kawaida huku wengine wakikesha kutoa huduma. 

Watu wanaendelea na shughuli zao za kijamii na kiuchumi licha ya baadhi ya maeneo ya jiji kushuhudia changamoto za usafiri wa umma kutokana na uchache wa magari. Sehemu kubwa ya barabara zina msongamano hafifu kiasi cha kuchukua muda mfupi kufika sehemu inayoenda. 

Ulinzi umekuwa ukiimarishwa siku hadi siku kuelekea siku ya leo Julai 7, ambayo ilipangwa kufanyika kwa maandamano.

Serikali imepiga maarufuku maandamano hayo wakiyataja kuwa ni vurugu zisizotambulika kisheria kwa kuwa hayakufuata sheria na taratibu za kuandaa na kufanya maandamano nchini.

Hali ilivyokuwa katika baadhi ya mitaa ya maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam. Picha | Nukta Habari

Julai 4, 2026, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliwataka wananchi kupuuza wito wowote unaohamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, likisisitiza kuwa halitakuwa tayari kumlinda yeyote atakayejihusisha na vitendo hivyo.

Siku moja baadaye, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, aliwaambia wanahabari katika Maonesho ya Sabasaba kuwa kuna baadhi ya wahamasisha wamekamatwa na uchunguzi dhidi yao upo mwishoni ili wachukulie hatua za kisheria. Hakutaja idadi kamili ya waliokamatwa. 

Misime alieleza Julai 5 kuwa baadhi ya wanaohamasisha maandamano hao wamepanga kufanya uhalifu mwingine ikiwemo kuwaua viongozi na wananchi, kuchoma shule na kupora mali za umma na watu binafsi. 

Hata hivyo, baadhi ya machapisho mtandaoni yalidai kuwa maandamano hayo, yasiyokuwa na kiongozi, yalipangwa kufanyika kwa amani. 

Hali ilivyokuwa katika baadhi ya mitaa ya Tegeta Mbuyuni jijini Dar es Salaam. Picha | Nukta Habari

Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi jana aliwataka Watanzania kuendelea na shughuli zao za kijamii na kiuchumi na kwamba Serikali itachukua hatua stahiki kwa yeyote atakayetishia au kufanya uhalifu au kutowesha amani. 

“Kwenye kila maeneo tutaendelea kuimarisha ulinzi na usalama ili kuhakikisha kila raia anastahili kwenda kufanya shughuli za uchumi aende, kwenye maeneo ya biashara kama kawaida, kote tupo,” alisema Katambi kwenye mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV