Ilemela wajenga madarasa 110 kupokea kidato cha kwanza

December 23, 2022 1:52 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Moja ya darasa lililozinduliwa leo ambalo litatumika na wanafunzi wa kidato cha kwanza katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemelea mkoani Mwanza. Picha | Mariam John.


  • Wanafunzi 12,548 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika Halmashauri hiyo hawatakosa sehemu ya kusomea.
  • Halmashauri yao yatumia Sh2.2 bilioni kukamilisha madarasa hayo. 

Mwanza. Wanafunzi 12,548 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika Halmashauri ya Manspaa ya Ilemela hawatakosa sehemu ya kusomea baada ya halmashauri hiyo kukamilisha vyumba vya madarasa 110 vilivyokuwa vinahitajika kwa ajilia ya wanafunzi hao.

Jumla ya Sh2.2 bilioni fedha kutoka Serikali Kuu zimetumika kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo sanjari na samani zake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo,  Mhandisi Modest Apolinary amesema walipokea kiasi hicho kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 110 na ununuzi wa viti na meza 5,500 pamoja na ofisi tatu.

” Lengo ni kuwawezesha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2023, kupata nafasi na kuanza masomo kwa wakati pamoja na kuwa na mazingira bora ya kujifunza na kujifunzia,” amesema Alponary leo Desemba 23,2022 wakati wa kukabidhi vyumba hivyo. 

Pamoja na kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo, halmashauri hiyo ilikuwa na uhitaji wa vyumba 252 kwa ajili ya wanafunzi hao na vilivyokuwepo ni vyumba 142 hivyo kufanya halmashauri hiyo kutokuwa na upungufu.

Mhandisi Apolinary amesema jamii pia ilishiriki katika mradi huo kwa kusaidia kutoa viashiria na nguvu kazi ambavyo vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya milioni 12, kama ishara ya kuunga juhudi ya Serikali.

“Tumeweza kutoa ajira fupi kwa wananchi 1,412, tumeweza kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, tumewezesha Serikali kupata kodi kutoka kwa mafundi na wazabuni waliouza vifaa vyao katika ujenzi huo,” amesema.

Pamoja na kufanikiwa kukamilisha ujenzi huo lakini wamekutana na changamoto ya kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi, kukatika kwa umeme na upatikanaji wa maji.


Soma zaidi


Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Massala, amesema kazi ya ujenzi wa vyumba hivyo wameifanya takriban siku 45 hadi 50.

“Wakati tunapewa fedha, tulipewa siku 75. Katika siku hizo wiki mbili Ilemela sisi tulikuwa bado hatujaanza kazi kwa sababu za kimfumo tulichelewa, lakini  tulianza maandalizi mengine na tulipoanza kulikuwa hakuna kusimama mpaka leo hii tunapokamilisha hii kazi,” amesema Massala.

Amesema mbali na fedha hizo kutoka Serikali Kuu, pia kuna vyumba 126 vilijengwa na nguvu ya wananchi na wamevikamilishwa kupitia fefha za mapato ya ndani.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya amesema huo ulipatiwa Sh19.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 983.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, amesema kukamilika kwa madarasa hayo ni mafanikio ya miaka miwili ya Rais ambapo mwaka jana pia walipokea madarasa kama hayo yaliyotokana na fedha za Uviko-19.

“Katika Wilaya zote 7 za Mkoa wa Mwanza Ilemela mmewakanyaga wenzangu vibaya sana, wengine hata ukiwauliza nyie mnakabidhi lini madarasa lugha zinakuwa zinapiga chenga, hivyo Ilemela nawapongeza sana,”  ameeleza Malima.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV