Wahamiaji haramu waongezeka kwa asilimia 112 ndani ya mwaka mmoja

May 25, 2026 5:18 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Idadi hiyo imeongezeka kutoka watuhumiwa 49,469 kwa mwaka 2026/27.
  • Serikali yaendelea kuimarisha operesheni za misako, doria na ukaguzi katika maeneo ya mipakani. 

Dar es Salaam. Idadi ya wahamiaji haramu waliokamatwa nchini imeongezeka kwa asilimia 112 ndani ya mwaka mmoja licha ya Serikali kuimarisha operesheni za misako, doria na ukaguzi katika maeneo ya mipakani. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi aliyekuwa akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni jijini Dodoma leo Mei 25, 2026, amesema Wizara kupitia Idara ya Uhamiaji imekamata watuhumiwa 49,469 hadi kufikia Aprili 2026.

Ongezeko hilo ni zaidi ya mara mbili ya kiwango cha watuhumiwa 23,315 waliokamatwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

“Kati ya hao wahamiaji haramu 34,099 waliokamatwa mwaka huu, waliondoshwa nchini,” ameeeleza Waziri Katambi

Uchambuzi wa Nukta Habari umebaini ongezeko la makundi ya wahamiaji hao haramu karibu kila mwaka.

Mathalani, mwaka 2025 kulikuwa na ongezeko la asilimia 31 kutoka watuhumiwa 17,791 waliokamatwa hadi Aprili 2024 ambapo kati yao 13,045 waliondoshwa nchini na kurudishwa katika nchi zao.

Licha ya ongezeko hilo, Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Pwani, SACI Dorah Luoga Februari 27 mwaka huu alisema pamoja na kuongezeka kwa wahamiaji haramu waliokamatwa, hali hiyo inaashiria kuimarika kwa udhibiti na si kuongezeka kwa tatizo. 

“Mwaka 2024 tulikamata wahamiaji haramu 958, huku mwaka 2025 idadi ikifikia 1,479, ongezeko hili limetokana na kuimarishwa kwa doria, misako na ushirikiano wa wananchi, jambo linalosaidia kuwabaini wanaoingia kupitia njia zisizo rasmi mapema na kuchukuliwa hatua za kisheria,” alieleza Luoga. 

Aidha, ili kukabiliana na wahamiaji haramu hususan katika mikoa ya mipakani, Wizara kupitia Idara ya Uhamiaji imeanzisha Kanda Maalum za Uhamiaji Mikoa ya Kagera na Kigoma ili kudhibiti wahamiaji haramu kwa kuongeza askari na vitendea kazi katika maeneo hayo. 

Waziri amesema kupitia bajeti ya Sh2.4 trilioni ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka 2026/27, idara itaendelea na misako, doria na kuanzisha kanda mpya katika maeneo ya kimkakati kudhibiti wahamiaji haramu. 

Kati ya fedha hizo Sh1.9 trilioni  sawa na asilimia 80 ya bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh1.1 trilioni  ni Mishahara na Sh7.6 bilioni ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV