Watalii waongezeka kwa asilimia 25.4 Tanzania
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ilishiriki katika mapokezi ya watalii 780 kutoka nchi ya Israel ambao waliwasili nchini Tanzania April 16, 2022 kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii. Watalii hawa walitumia ndege nne za kukodi ambazo zimefanya safari zake za moja kwa moja kutoka nchini ya Israel. Picha | Bodi ya Utalii (TTB).
- Mwaka unaoishia Machi 2023, Tanzania ilipokea watalii  118,186 ambao wameongezeka kutoka 93,889 waliorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2022.
Dar es Salaam. Idadi ya Watalii wanaotembelea Tanzania imeongezeka kwa asilimia 25.8 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi mwaka huu wa 2023.
Kwa mujibu wa taarifa za mara kwa mara (high-frequency data) zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), hadi kufikia mwaka unaoishia Machi 2023, Tanzania ilipokea watalii  118,186 ambao wameongezeka kutoka 93,889 waliorekodiwa kipindi kama hicho mwaka 2022.
Hilo ni sawa na ongezeko la watalii 24,297 (asilimia 24.8) ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.Â
Ripoti hiyo inaonyesha katika kipindi hicho, Julai 2022 ndiyo mwezi uliorekodi watalii wengi zaidi kuliko miezi mingine. Watalii waliotembelea Tanzania walikuwa 166,736.
Hata hivyo, tangu mwaka 2023 uanze, idadi ya watalii wanaokuja nchini imekuwa ikishuka mfululizo. Mathalan, Januari NBS ilirekodi watalii 146,877 na mwezi uliofuata walishuka hadi 144,019 kabla hawajashuka zaidi hadi 118,186 mwezi Machi.Â
Kutokana na hatua mbalimbali inazochukua Serikali, huenda idadi ya watalii wanaokuja nchi ikaongezeka zaidi kuliko ile ya mwaka 2022. Hatua hizo ni pamoja kuboresha na kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwa njia mbalimbali ikiwemo matangazo ya kidijitali na filamu ya ‘Royal Tour’.Â
