Idadi ya watalii yapaa kwa asilimia 27 Tanzania

May 11, 2024 6:33 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yafikia 520,324 katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024.
  • Marekani, Italia, Kenya na Burundi zaongoza kuingiza watalii wengi.

Dar es Salaam. Idadi watalii wanaotembelea nchini Tanzania imepaa kwa asilimia 27.2 katika kipindi cha mwaka mmoja jambo linalotoa fursa kwa wadau wa utalii nchini na Taifa kujipatia fedha za kigeni zitakazochangia kukua kwa uchumi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa Takwimu (NBS) idadi ya watalii walioingia nchini imepaa hadi 520,324 katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024, ikilinganishwa na watalii 409,082 walioingia nchini katika kipindi kama hicho mwaka 2023.

“Idadi hiyo ya watalii waliongia nchini mwaka huu ni ongezeko la 111,242 sawa na asilimia 27.2,” imesema Taarifa Nbs iliyotolewa Mei 10, 2024.

Uchambuzi zaidi wa takwimu hizo za NBS unaonyesha kuwa idadii hiyo ya watalii wanaoingia nchini katika kipindi cha Januari hadi Machi imekuwa ikiongezeka kwa miaka minne mfululizo.

Mwaka 2022 watalii 289,372 waliingia nchini ikiongezeka kutoka watalii waliongia 231,131 nchini mwaka 2021. 

NBS inabainisha kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuingiza  idadi kubwa ya watalii ni pamoja Italia, Ufaransa na Marekani rekodi ambayo nchi hizo imeishikilia kwa muda mrefu.

Barani Afrika nchi za Burundi, Kenya na Zambia zinaongoza kwa kuingiza watalii wengi nchini.

Enable Notifications OK No thanks