Fursa zilizojificha utalii wa milimani

June 29, 2023 8:25 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Fursa ya kutembea, kupanda milima na kuendesha baiskeli nayo inakusubiri ili kujionea uzuri uliopo katika msitu wa Magoroto mkoani Tanga ambao unatajwa kama pepo ya aina yake Tanzania. Picha| K15 Photos.


  • Unaweza kuwasaidia wenyeji kujipatia kipato na kutunza mazingira.
  • Bado watu wengi hawajui kwa undani utalii huo
  • UN yazitaka Serikali kuungana kuboresha utalii huo ili kukuza uchumi wa dunia. 

Dar es Salaam. Utalii wa milimani ukisimamiwa kwa uendelevu, una uwezo wa kukuza kipato cha jamii zinazozunguka rasilimali hizo na kusaidia kuhifadhi maliasili na utamaduni wao, yameeleza mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN).

Hata hivyo, ukosefu wa data na ujuzi kuhusu rasilimali hiyo kunawazui watu wa maeneo husika kufaidika kikamilifu na fursa vivutio hivyo vya utalii.

Ripoti iliyochapishwa Aprili 26, 2023 na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na Ushirikiano wa Milimani (MP) inataka kushughulikia mapungufu hayo ili kufikia uelewa mzuri wa fursa hiyo. 

Ripoti hiyo hiyo pia inabainisha mienendo na kutoa mapendekezo kadhaa ya kuendeleza upimaji wa utalii wa milimani, ikijumuisha maendeleo ya takwimu rasmi za utalii na matumizi ya data kubwa na teknolojia mpya.

Milima ni nyumbani kwa karibu watu bilioni 1.1, baadhi yao wakiwa maskini zaidi na waliotengwa zaidi ulimwenguni.

Wakati huo huo, milima imevutia kwa muda mrefu kutembea, kupanda na washabiki wa michezo ya msimu wa baridi. Pia huvutia wageni kwa mandhari ya kuvutia, viumbe hai na tamaduni za wenyeji.

Hata hivyo, mwaka wa 2019, nchi 10 ikiwemo China na Uholanzi zenye milima mingi zilipokea asilimia 8 tu ya watalii wa kimataifa, inasema ripoti hiyo, yenye kichwa “Kuelewa na Kupima Utalii wa milimani.”

“Kupima idadi ya wageni wanaotembelea milimani ni hatua ya kwanza muhimu tunayohitaji kuchukua. 

“Kwa data sahihi, tunaweza kudhibiti vyema usambaaji wa mtiririko wa wageni, kusaidia upangaji wa kutosha, kuboresha ujuzi juu ya mifumo ya wageni, kujenga bidhaa endelevu kulingana na watumiaji na kuunda sera zinazofaa ambazo zitakuza maendeleo endelevu na kuhakikisha shughuli za utalii zinanufaisha jamii za wenyeji,” Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu na Katibu Mkuu wa UNWTO Zurab Pololikashvili wameandika katika dibaji ya ripoti hiyo.


Zinazohusiana: 


Utalii wa milimani unakadiriwa kuchangia asilimia 9 hadi 16 ya watalii wa kimataifa kila mwaka sawa wastani wa watalii kati ya milioni 195 na milioni 375 wanaotembelea vivutio mbalimbali duniani.

Uhaba wa data kuhusiana na utalii wa ndani haukufanya iwezekane kukadiria mchango wa utalii huo katika ukuaji wa uchumi wa dunia. 

Utalii umethibitika kuwa tegemeo kwa jamii nyingi katika maeneo ya milimani na unaweza kuchukua jukumu kuu katika kulinda njia za kujipatia riziki zinazokubalika kwa mifumo ya ikolojia, ambayo inakabiliwa na vitisho vinavyoendelea kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Inapendekeza juhudi za pamoja, zinazohusisha wadau wa umma na binafsi katika mnyororo wa thamani, kuboresha ukusanyaji wa takwimu, viwango na utoaji ili kupata tathmini ya kina zaidi ya utalii wa milimani kwa kuzingatia wingi na athari zake, ili uweze kueleweka na kuendelezwa zaidi. 

Ripoti hiyo pia inataka kazi ya pamoja ili kusaidia kuongeza ufahamu wa umuhimu wa kijamii na kiuchumi wa utalii katika milima na sera zinazolengwa za kuunda nafasi za kazi, kusaidia biashara ndogo na za kati na kuvutia uwekezaji wa kijani katika miundombinu na uwekaji wa huduma za utalii kidijitali.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW