Serikali yakaribisha wawekezaji binafsi  pori la akiba Pande kukuza utalii

January 28, 2025 6:16 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Serikali imewatoa wito kwa wawekezaji binafsi kujiunga na juhudi za kuendeleza pori pekee la akiba la Pande lililopo jiji la Dar es Salaam ili kuchochea shughuli za utalii.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula, wakati akijibu swali la Mbunge viti maalum Dar es Salaam, Mariam Kisangi  katika mkutano wa Bunge la 12, kikao cha kwanza cha mwaka 2025.

Kitandula amesema kuwa wizara imetenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji katika miundombinu ya michezo ya watoto, huduma za malazi, na vivutio vingine vya utalii, na kuwataka wawekezaji kuchukua fursa hiyo.

“Tunatoa fursa kwa wawekezaji kujenga miundombinu ya malazi na huduma zingine ndani ya eneo hili, pamoja na kuendelea kuongeza idadi ya wanyama taratibu kulingana na uwezo wa ikolojia,” amesema.

Sekta ya utalii nchini Tanzania ina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa, ikiwa ni pamoja na kuchangia asilimia 21.5 ya pato la taifa (GDP) na asilimia 30.9 ya mapato ya fedha za kigeni. 

Kulingana na makadirio ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2023/24, utalii pekee unachangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni, huku misitu na nyuki zikichangia asilimia 5.9.

Wawekezaji binafsi guenda wakasaidia kulifanya Pori la Pande kuwa kivutio kikubwa zaidi cha utalii kwa kujenga miundombinu ya malazi, michezo, na huduma zingine zinazowafaa watalii ili kuwavutia wengi zaidi na kuchangia zaidi katika uchumi wa taifa.

Kitandula ameongeza kuwa tayari Serikali imefanya miradi kadhaa ya kuiboresha hifadhi hiyo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kupumzikia wageni, kambi za watoto, na bustani ya wanyama wa pori. 

“Kuanzia mwaka wa fedha 2021/22, tumejenga miundombinu mikubwa, na mwaka 2023/24 tumeanzisha bustani ya wanyama pori ambapo kwa sasa kuna zaidi ya wanyama 100, ikiwa ni pamoja na duma, mamba, simba, pundamilia, na nyoka wa aina mbalimbali,” amesema Kitandula.

Aidha, amebainisha kuwa miundombinu ya barabara imeboreshwa na lango kuu la kuingilia pori limejengwa, jambo lililochangia kuongezeka kwa idadi ya watalii. 

“Kuanzia 2023 hadi 2024, watalii 4,606 wametembelea pori hilo, na tunaendelea kuifanya hifadhi hii kuwa kivutio kikubwa zaidi,” ameongeza.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 96, kutoka 922,692 mwaka 2021 hadi 1,808,205 mwaka 2023. 

Vilevile, idadi ya watalii wa ndani imeongezeka kwa asilimia 152, kutoka 788,933 mwaka 2021 hadi 1,985,707 mwaka 2023. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.