Jinsi ya kujikinga na Corona unaposheherekea Krismasi
- Chagua sehemu ambayo ina uwazi wa kutosha.
- Zingatia kwenda sehemu inayoheshimu tahadhari za Corona.
- Kama hakuna ulazima, sherehekea nyumbani na familia yako.
Dar es Salaam. Msimu wa sikukuu ni msimu wa furaha. Amani inaanza na kuwaona ndugu, familia kuunganika na wazazi kuwa nyumbani baada ya kufanya kazi kwa mwaka mzima.
Hivyo ni kati ya vitu vinavyoleta tabasamu kwa watoto, ndugu na wazazi nyumbani.
Hata hivyo, inapofika siku ya sikukuu huenda wazazi na walezi wakawa na njiapanda ya sehemu ya kwenda kujivinjari iwe ni kwa ajili ya kupata chakula cha mchana na hata kutembea tu baada ya mlo wa nyumbani.
Unapotaka kufanya maamuzi ya sehemu ya kwenda, ni vyema kuzingatia baadhi ya vitu ili kuilinda familia yako na ugonjwa wa Corona ambao bado unasumbua sehemu mbalimbali duniani.
Kati ya vitu vya kuzingatia ni kuchagua sehemu ya wazi na inayozingatia tahadhari dhidi ya Corona.
Uzingatie nini kingine? Mambo yote kwenye video hii.
Latest