Madarasa ya ghorofa yatakavyomaliza tatizo la ardhi Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akimwonyesha Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngussa Samike mwonekano wa ujenzi wa mradi wa vyumba vya madarasa ya gorofa ambayo wilaya hiyo imeanza kutekeleza ili kuendana na ufinyu wa rasilimali ya ardhi. Picha|Mariam John.
- Halmashauri ya jiji la Mwanza imeanza kujenga vyumba vya madarasa vya ghorofa.
- Hatua hiyo inapunguza changamoto ya ukosefu wa ardhi ya ujenzi.
- Pia inawawekea wanafunzi mazingira rafiki ya kusomea.
Mwanza. Halmashauri ya jiji la Mwanza imeanza kujenga majengo 13 ya vyumba vya madarasa vya ghorofa vitakayokuwa na jumla ya vyumba 64 katika shule za sekondari ili kupunguza gharama za manunuzi ya ardhi.
Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Sekiete Yahya akitoa taarifa ya ujenzi wa madarasa yaliyotokana na fedha za mgao wa Sh1.3 trilioni ambazo Tanzania ilipewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambazo Tanzania.
Halmashauri hiyo ilipokea Sh1.69 bilioni kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa 98.
Kutokana na matumizi ya ardhi katika jiji la Mwanza kuendelea kuwa adimu, halmashauri hiyo kwa kushirikiana na kamati ya ujenzi walikubaliana kujenga maghorofa ili kutumia ardhi iliyopo kujenga vyumba vingi vya madarasa.
Amesema kati ya fedha hizo walizopewa zilifanikisha kujenga vyumba 39 vya kawaida kwa gharama ya Sh780 milioni pamoja na samani zake zake za ndani huku kiasi cha fedha kilichobaki halmashauri kupitia mapato yake ya ndani waliongezea Sh1.5 bilioni ili kujenga vyumba 64 vya maghorofa.
“Jiji la Mwanza linakua na linahitaji kuboreshwa hivyo mradi huu wa magorofa utakuwa na manufaa makubwa na utapendezesha madhari ya jiji hilo,” amesema Yahya.
Mbinu hiyo ya kujenga madarasa ya ghrofa itasaidia wanafunzi kupata mazingira sahihi ya kusomea na hivyo kuwapunguzia maumivi wanafunzi kusoma mbali na maeneo yao.
Zinazohusiana:
- Mbinu zitakazowasaidia watahiniwa darasa la saba kufanya vizuri.
- Necta yafuta matokeo ya watahiniwa 909 darasa la saba
- Kanda ya ziwa yatikisa matokeo darasa la saba 2019
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na kumuomba kuiomba awapatie fedha zingine kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule ya msingi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema wilaya hiyo ilifaulisha zaidi ya wanafunzi 1,000 watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu na wote watapata fursa kuanza shule kwa pamoja kwa sababu wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngussa Samike amepongeza ubunifu waliofanya jiji la Mwanza kwa kuzingatia matumizi ya ardhi na kwamba majengo hayo yataendelea kupandisha hadhi ya jiji hilo.
“Nipongeze kwa ubunifu huu, vyumba hivi havina gharama na sasa jiji la Mwanza mtalazimika kujenga vyumba 103 vya madarasa badala ya 98 kama fedha za Uviko-19 zilivyoelekezwa,” amesema Samike.
Kwa mujibu wa Katibu Tawala huyo, Mkoa wa Mwanza ulipokea Sh20.5 bilioni za Uviko-19 ambazo zingetosha kujenga vyumba vya madarasa 1,017.
Pia ameagiza madarasa hayo ghorofa yawekewe miundombinu rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu ili kuwawezesha kusoma bila vikwazo.
Hivi karibuni akiwa jijini Mwanza, Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi alilipongeza jiji hilo kwa mpango huo na kuagiza Mamlaka zote za upangaji miji kwenda namna hiyo kwa kujifunza Mwanza.
Waziri Lukuvi alisema ni aibu kusema ardhi imejaa na ardhi ni rasilimali muhimu lazima ilindwe na kwa sasa mpango uliopo ni kujenga majengo kwenda juu na hiyo ndiyo sayansi.
Latest