Bei ya viazi mviringo yapanda Arusha

January 10, 2022 1:23 pm · Maria
Share
Tweet
Copy Link
  • Imepanda kutoka Sh90,000 hadi Sh100,000 katika kipindi cha wiki moja. 
  • Wafanyabiashara mkoani watapata faida ya Sh10,000 kwa kila gunia moja la kilo 100.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa viazi mviringo katika Mkoa wa Arusha leo watalala na tabasamu baada ya bei ya jumla ya zao hilo kupanda kwa Sh10,000 ndani ya kipindi cha wiki moja. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Januari 10, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo linauzwa kwa Sh100,000 mkoani humo.

Bei hiyo imepanda kutoka Sh90,000 iliyorekodiwa Jumatatu Januari 03, 2022, sawa na kusema wafanyabiashara wataweka kipindoni Sh10,000 kwa kila gunia moja watakalouza leo sokoni. 

Pia takwimu hizo ambazo hutolewa mara tatu kwa wiki, zinaonyesha kuwa bei ya chini ya viazi mkoani humo imepanda hadi Sh95,000 kutoka Sh80,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita. 

Kwa bei hizo zinazotumika leo, itakuwa ni maumivu kwa wanunuzi na kicheko kwa wafanyabiashara ambao kupanda kwa bei za mazao ndiyo faida kwao. 

Licha ya kuwa bei ya juu na chini ya viazi mviringo katika Mkoa wa Arusha kupanda, bei ya juu kabisa ya zao hilo inayotumika leo kwa upande wa Tanzania Bara imerekodiwa mkoani humo pamoja na Mwanza na Lindi  ambayo ni Sh100,000 huku bei ya chini ni Sh50,000 katika Mkoa wa Njombe na Dodoma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Nukta TV

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Nukta TV

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Nukta TV