Neema kwa wafanyabiashara bei ya mchele ikipanda Dar

September 23, 2022 5:49 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya juu ya gunia la kilo 100 kwenye soko la Temeke mkoani humo ni Sh320,000 kutoka Sh280,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita.
  • Wakati bei ya juu ikiongezeka, bei ya chini ya zao hilo nayo imeongezeka  kwa Sh10,000 na kufikia Sh 250,000.

Dar es Salaam. Bei ya jumla ya mchele katika jiji la Dar es Salaam imepanda kwa Sh50,000 ndani ya kipindi cha wiki moja, jambo linalowafaidisha wakulima waliopeleka zao hilo jijini humo.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa leo (Septemba 23, 2022) na Wizara ya Viwanda na Biashara  zinaonyesha kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo jijini humo ni Sh330,000 katika soko la Temeke.

Bei hiyo imepanda kutoka Sh280,00  iliyorekodiwa Ijumaa ya Septemba 16 mwaka huu.

Kupanda kwa bei hiyo ya juu kutawanufaisha zaidi wafanyabiashara na wakulima huku wanunuzi wakitoboa mifuko yao kwa Sh50,000 zaidi kwa kila gunia moja iwapo hesabu hizo zitapigwa kwa bei ya juu.

Aidha takwimu hizo zinaonyesha kuwa bei ya chini ya zao hilo la chakula inayotumika leo imerekodiwa mkoani Iringa ambapo ni Sh 170,000, ambayo haijabadilika tangu wiki iliyopita.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Wamiliki wa 'Guest House, Lodge' sajilini kila anayeingia kwa NIDA

Nukta TV

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Ndejembi: Watanzania wataanza kuona bei ya mafuta ikishuka

Nukta TV

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Katambi asitisha mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa TANZANIA

Nukta TV