Lindi yafunika bei ya viazi mviringo
- Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya Lindi linauzwa kwa Sh120,000.
- Bei ndiyo bei ya juu kabisa Tanzania Bara.
- Bei ya chini ya zao hilo ni Sh46,000 inayotumika mkoani Njombe.
Dar es Salaam. Watumiaji wa viazi mviringo hasa kutengeneza chipsi katika Mkoa wa Lindi leo watalala na maumivu kutokana na bei ya jumla ya zao hilo kuuzwa kwa bei ya juu kuliko maeneo mengine Tanzania Bara.
Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara leo (Januari 31, 2022) zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya Lindi linauzwa kwa Sh120,000.
Bei hiyo ni mara mbili zaidi ya bei inayotumika katika masoko ya Njombe ambayo ni Sh46,000, jambo linalowanufaisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka bidhaa hiyo mkoani humo.
Bei hiyo inayotumika Lindi ndiyo bei ya juu Zaidi huku ya Njombe ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei zinazotumika katika maeneo mengine nchini.
Viazi mviringo ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula ambavyo vimekuwa vikitumiwa kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kukaanga chipsi ambazo zinapendwa zaidi na mabachela.
Latest



