Mwelekeo mpya sekta ya utalii Tanzania

March 31, 2022 7:35 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuimarisha uhifadhi na vivutio vya utalii.
  • Serikali kuongeza kasi ya kuwahudumia wawekezaji.

Dar es Salaam. Huenda sekta ya utalii Tanzania ikapata msukumo mpya kutoka katika athari za janga la Corona (Uviko-19) mwaka mmoja uliopita baada ya Serikali kuongeza kasi ya utoaji wa vibali na leseni za uwekezaji.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi  kwa wawekezaji wa sekta ya utalii pamoja na kuendelea kuboresha  huduma za kitalii ikiwemo upatikanaji wa leseni ya shughuli za utalii kwa haraka pamoja na mifumo ya malazi.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kutoa fursa katika maeneo yaliyohifadhiwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi.

“Sisi kama Wizara ya Maliasili na Utalii, falsafa yetu ni moja tu, mteja ni mfalme. Ndiyo maana mimi, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, tuko tayari kukutana na mwekezaji wa aina yoyote yule, muda wowote ule kujadili changamoto zozote zile, milango iko wazi,” amesema.

Dk Ndumbaro amesema  hayo  leo Machi 31, 2022 jijini Dar Es Salaam  wakati akikabidhi vyeti kwa wawekezaji waliokidhi vigezo na  kufanikiwa kupata maeneo ya uwekezaji mahiri katika maeneo ya wanyamapori (SWICA), yanayosimamiwa na   Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambao ni  kampuni mbili  za  Grumet  Services Ltd pamoja na Mwiba Holding ltd.

Amewasisitiza wawekezaji wazawa pamoja na wa kigeni kulinda na kutangaza utalii na  maeneo ya uhifadhi na vivutio hapa nchini, katika maeneo waliyopewa kuwekeza kwa kushirikiana na Serikali.


Zinazohusiana:


Pia Waziri Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wawekezaji wa kigeni kuwekeza nchini, akiitaja Tanzania kuwa ni salama yenye amani na demokrasia na kwamba wizara anayoiongoza imefungua milango kwa wawekezaji wote kuja kuwekeza nchini.

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo,  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Grumeti Reserves Ltd, Graham Ledger amesema kampuni ya Grumeti inashukuru kupata cheti cha umiliki wa vitalu viwili kwa sasa na  inaahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kulinda na kuendeleza shughuli za uhifadhi nchini.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mwiba Holding ltd., Mark Ghaui ameishukuru Serikali kwa juhudi inazofanya kuhakikisha shughuli za uhifadhi zinaleta tija kwa Taifa  kwa kuhakikisha unaimarika kwa kuleta faida ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi kwa kupitia uwekezaji huo wa muda mrefu.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV