WHO: Uviko-19 bado unasambaa kwa kasi duniani

January 5, 2023 8:19 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Yataka mjadala na hatua zaidi za kinga na kitabibu zinapaswa kuendelea kuchukuliwa duniani kote. 

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema ingawa idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa Uviko-19 ilipungua kwa mwaka 2022, bado tishio la ugonjwa huo linaendelea kwa mwaka huu.

WHO imesema kutokana na hali hiyo, mjadala na hatua zaidi za kinga na kitabibu zinapaswa kuendelea kuchukuliwa duniani kote. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Ghebreyesus amesema mwaka huu ikiwa ni wa nne tangu Uviko-19 kutangazwa, hatua kubwa imepigwa katika upatikanaji wa chanjo, matibabu na usimamizi wa ugonjwa huo lich ya changamoto mbalimbali.

“Bado kuna ukosefu wa uwiano katika kupima, kutibu na chanjo na ndipo Uviko-19 inasalia kuwa tishio kwa afya, uchumi na jamii. Kila wiki takribani watu 10,000 wanakufa duniani kwa Uviko-19, idadi ambayo ndio inatufikia. Idadi halisi inaweza kuwa kubwa,” amesema Dk Tedros. 

Amesema  hofu yao kubwa zaidi ni taswira ya ugonjwa huo kutokana na kasi ya maambukizi kwenye maeneo mengi duniani na mnyumbuliko wa lahaja za virusi. 

“Katika wiki za karibuni kumekuweko na ripoti za ongezeko la wagonjwa wanaolazwa kutokana na Uviko-19, hospitali kuzidiwa uwezo hasa katika maeneo ya kaskazini mwa dunia ambako magonjwa ya njia ya hewa ikiwemo homa ya mafua yanasambaa,” amefafanua mkuu huyo wa WHO. 


Soma zaidi:


China nako idadi ya wagonjwa wanaolazwa kutokana na Uviko-19 inaongezeka na “tumeendelea kuisihi China itupatie kwa kasi kubwa takwimu sahihi kuhusu wanaolazwa na vifo.” 

Dkt. Tedros amesema takwimu sahihi ni muhimu kwa WHO kuweza kufanya kazi yake na hivyo amesihi kila nchi ifanye hivyo. 

Mwishoni mwa mwaka 2022, Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu aliwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari ikiwemo kupata chanjo kwa sababu ugonjwa huo bado upo na maambukizi yameendelea kuongezeka. 

Amezungumzia pia Ebola nchini Uganda akisema hakujakuweko na ripoti zozote za kupatikana kwa mgonjwa mpya tangu Novemba 27, 2022 na iwapo hali hiyo itaendelea basi ifikapo Januari 11, 2023, mlipuko wa Ebola nchini Uganda utatangazwa kuwa umemalizika.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW