Watatu wafariki katika mlipuko wa ‘hantavirus’ ndani ya meli ya kitalii

May 4, 2026 6:43 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Abiria wawili wenye dalili wanatarajiwa kuhamishwa kwa matibabu maalumu.
  • Maofisa wa afya waendelea kufuatilia uwezekano wa maambukizi zaidi ndani ya meli.

Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha vifo vya watu watatu kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa hantavirus ulioripotiwa ndani ya meli ya kitalii MV Hondius iliyokuwa ikisafiri katika Bahari ya Atlantiki kutoka Argentina kuelekea Cape Verde.

Kwa mujibu wa taarifa WHO iliyotolewa Mei 3, 2026 tayari kisa kimoja cha maambukizi hayo kimethibitishwa kupitia vipimo vya maabara huku visa vingine vitabo vikihisiwa kuwa vya ‘hantavirus’. 

“Kati ya watu sita walioathirika, watatu wamefariki dunia na mmoja anaendelea kupatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) nchini Afrika Kusini…

…WHO inaendelea kusaidia uchunguzi wa kina wa maabara, uchunguzi wa mwenendo wa maambukizi pamoja na utoaji wa huduma za matibabu kwa abiria na wahudumu wa meli,” sehemu ya taarifa ya WHO imeeleza.

Hantavirus‘ ni kundi la virusi hatari vinavyoenezwa na panya (mkojo, kinyesi, au mate) na vinaweza kusababisha magonjwa makali ya mapafu (HPS) au figo kwa binadamu. Maambukizi hutokea kwa kuvuta hewa yenye vumbi la kinyesi cha panya. 

Ingawa maambukizi kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni nadra kutokea, virusi hivyo vinaweza kusababisha ugonjwa mkali wa mfumo wa upumuaji unaohitaji uangalizi maalumu wa kitabibu.

Taarifa zilizotolewa na shirika hilo zinaeleza kuwa mwanaume mwenye umri wa miaka 70 raia wa Uholanzi alianza kuonesha dalili za ugonjwa huo akiwa ndani ya meli hiyo kabla ya kufariki dunia. 

Mke wake, ambaye pia alipata dalili zinazofanana na hantavirus, alifariki dunia akiwa amelazwa katika hospitali moja jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Aidha, mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 69 raia wa Uingereza anaendelea kupatiwa matibabu katika ICU huku hali yake ikielezwa kuwa mbaya.

Katika tukio hilo, wahudumu wawili wa meli hiyo pia wamewekwa chini ya uangalizi wa karibu wa kitabibu baada ya kuonesha dalili zinazohusishwa na maambukizi hayo.

Aidha, WHO imesema inaendelea kushirikiana kwa karibu na Nchi Wanachama pamoja na waendeshaji wa meli hiyo katika kuratibu hatua za kudhibiti maambukizi hayo, ikiwemo uhamishaji wa kitabibu wa abiria wawili wenye dalili za ugonjwa huo pamoja na kufanya tathmini ya kina ya hatari kwa afya ya umma.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa X amesema hatua za haraka na zenye uratibu ni muhimu ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na kulinda afya ya umma.

Wakati huo huo, kupitia vyombo vya habari vya kimataifa, mamlaka za Uholanzi zimesema zinaendelea kufanya maandalizi ya kuwarejesha nchini humo watu wawili wenye dalili pamoja na miili ya marehemu kwa ajili ya taratibu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Utani wa Spika Zungu, akimtambulisha Didier Drogba Bungeni leo

Utani wa Spika Zungu, akimtambulisha Didier Drogba Bungeni leo

Nukta TV

🔴LIVE: MAKONDA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI | Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

🔴LIVE: MAKONDA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI | Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

Nukta TV

🔴LIVE: KAIRUKI AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI

🔴LIVE: KAIRUKI AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI

Nukta TV