Wanafunzi darasa la saba kuanza mtihani wa Taifa kesho

October 4, 2022 1:54 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Mitihani hiyo itafanyika kwa siku mbili Oktoba 5 hadi 6, 2022 nchi nzima.
  • Watahiniwa milioni 1.4 wa darasa la saba wanatarajia kuanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kesho.

Dar es Salaam. Watahiniwa milioni 1.4 wa darasa la saba wanatarajia kuanza mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kesho, ikiwa ni daraja muhimu kujiunga na sekondari. 

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) mitihani hiyo itafanyika kwa siku mbili Oktoba 5 hadi 6, 2022 nchi nzima.

Necta imesema kati ya watahiniwa hao, 723,064 ni wasichana sawa na asilimia 52 ya watahiniwa wote.

Idadi ya watahiniwa hao imeongezeka kwa asilimia 22 kutoka milioni 1.1 wa mwaka 2021.

“Aidha, jumla watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 4,221, miongoni mwao 101 ni vipofu,  1,198 wasioona vizuri, viziwi 962, walemavu wa akili 487 na walemavu wa viungo 1,473,” amesema Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Athumani Amasi.

Mtihani huo utahusisha jumla ya masomo matano ambayo ni Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Kiswahili, Lugha ya Kiingereza, na Maarifa ya Jamii.

Kwa mujibu wa Necta, ufaulu wa jumla wa wanafunzi katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana ulikuwa 81.97 huku wanafunzi 393 walifutiwa matokeo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV