Usidanganyike! Pilipili hazitibu ugonjwa wa Corona
- Ingawa pilipili ni zao linalotumika kuongeza ladha kwenye chakula lakini haitibu au kuzuia COVID-19.
- Njia rahisi ya kujikinga na Corona ni kukaa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine, kunawa mikono mara kwa mara na kutumia kitakasa mikono.
Dar es Salaam. Katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa corona habari nyingi za uzushi zimesikika kuhusu namna ya kijitibu na maradhi hayo.
Moja ya uzushi huo ni baadhi ya watu kudai kuwa matumizi ya pilipili kwenye supu na vyakula vingine yanasaidia kutibu ugonjwa wa COVID-19.
Kama umekutana au kusoma habari kama hiyo, fahamu kuwa haina ukweli wowote kwa sababu pilipili haitibu ugonjwa huo na hadi sasa kinachofahamika ni kwamba corona haitibiki bali madaktari hutibu tu dalili.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema ingawa pilipili ni zao linalotumika kuongeza ladha kwenye chakula lakini haitibu au kuzuia COVID-19.
“Kuongeza pilipili kwenye supu au vyakula vingine haizuii au kutibu COVID-19,” imeeleza WHO.
Zinazohusiana
- Ni uzushi: Huwezi kupata maambukizi ya Corona kwa kuchangia damu
- Ukweli kuhusu maiti kuambukiza Corona
Njia rahisi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ni kukaa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine, kunawa mikono mara kwa mara na kutumia kitakasa mikono.
WHO imesema ni muhimu kujenga afya bora kwa kula mlo kamili, maji ya kutosha, kufanya mazoezi na kupumzika.
Usikubali kupotoshwa. Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya Facebook/Twitter @NuktaFakti na Instagram @nuktafakti.
Latest
