Hapana: Kuosha pua kwa maji ya chumvi hakuzuii Corona

November 18, 2020 8:32 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Virusi vya ugonjwa wa Corona haviwezi kudhibitiwa kwa kuosha pua kwa maji yenye chumvi. 
  • Njia ya kujikinga na COVID-19 ni pamoja na kunawa mikono, kuvaa barakoa na kutumia kitakasa mikono.

Dar Es Salaam. Wakati wataalam wa afya wakiendelea na mapambano dhidi ya janga la Corona (COVID-19), bado habari za uzushi kuhusu ugonjwa huo zinaendelea kusambaa kwa kasi duniani. 

Miongoni mwa habari hizo za uzushi  zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ni zile zinazodai kuwa kuosha pua mara kwa mara kwa kutumia maji yenye chumvi ni njia mojawapo ya kumkinga mtu na maambukizi ya Corona

Hata hivyo, taarifa hizo hazina ukweli wowote, ni uongo ambao unalenga kuwapotosha watu. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema virusi aina ya COVID-19 haviwezi kudhibitiwa kwa kuosha pua kwa maji yenye chumvi.

“Hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa kuosha pua mara kwa mara kunaweza kumkinga mtu dhidi ya maambukizi ya Corona,” imesema  WHO. 

WHO inasisitiza kuwa njia pekee ya kujikinga na COVID-19 ni kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni; kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya; kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuvaa barakoa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV