Ukweli kuhusu maiti kuambukiza Corona

Rodgers George 0136Hrs   Juni 19, 2020 NuktaFakti
  • Hakuna ushahidi kuwa mwili wa mgonjwa wa Corona unaweza bado kueneza maambukizi saa mbili tangu kifo kilipotokea. 
  • Unashauriwa kuwasiliana na kituo cha kutolea huduma za afya na usioshe wala kuhifadhi mwili wa mtu aliyefariki kwa Corona nyumbani.

Dar es Salaam. Ugonjwa wa wa virusi vya Corona umeibua maswali mengi kwa watu hasa jinsi ya kujikinga huku wengine wakiamua kujipa majibu ya maswali yao na pengine bila kuwa na uhakika wa wanachokisema.

Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii, huenda umewahi kukutana na kuziamini habari kuhusu miili ya watu waliofariki kwa COVID-19 inaweza kueneza ugonjwa huo baada ya saa mbili, basi fahamu kuwa umedanganywa.

Wazira ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kituo chake cha mtandaoni cha taarifa za Corona imeeleza hakuna ushahidi kuwa mwili wa mgonjwa wa Corona unaweza bado kueneza maambukizi saa mbili tangu kifo kilipotokea. 


Zinazohusiana


Hata hivyo, wizara hiyo imeshauri watu kutokuhifadhi mwili wa mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Corona nyumbani wala kuuosha. 

Badalla yake, wawasiliane na wataalamu kwa ajili ya kupewa maelekezo muhimu.

“Usihifadhi mwili wa marehemu nyumbani, toa taarifa kituo cha kutolea huduma za afya kilichopo karibu. Pia Usiuguse wala kuosha mwili wa marehemu, Maziko yataratibiwa na wataalamu wa afya ili kuepuka maambukizi,” Imeeleza wizara hiyo.

Related Post