Hapana: Wanaovaa miwani hawana uwezekano mdogo wa kupata Corona

March 4, 2021 9:03 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakuna tafiti rasmi iliyothibitisha madai hayo. 
  • Taarifa zinazosambaa juu ya madai hayo ya kuvaa miwani kujikinga na Corona siyo ya kweli.
  • Watu washauriwa kupata sahihi za Corona kupitia WHO na Wizara ya Afya.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa miwani, huenda ulianza kujihisi mwenye bahati baada ya kukutana na taarifa zikidai kuwa watumiaji wa miwani wana uwezekano mdogo wa kuugua ugonjwa wa Corona.

Lakini huenda matarajio uliyonayo siyo sahihi kwa sababu taarifa hizo ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.

Habari hiyo inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Whatsapp na Twitter, kwa mfumo wa picha ya mtoto amevaa barakoa na miwani, imeambatanishwa na maandishi na kiunganishi kinachoelekeza kwenda kwenye taarifa husika.

Maandishi katika picha  hiyo yanasema “Coronavirus: Glasses wearers less likely to get COVID.” yakimaanisha “Wavaaji wa miwani wana uwezekano mdogo wa kuugua Corona.”

Hata hivyo, habari hiyo haina ukweli wowote kwasababu hakuna tafiti yoyote rasmi iliyothibitisha madai hayo.

Pia tovuti inayochapisha machapisho ambayo hayajarasimishwa iitwayo Medrixiv imeeleza juu ya tafiti iliyofanyika India inayosema watumiaji wa miwani hawana asilimia kubwa ya kuugua Corona, lakini bado madai hayo yameonekana kuwa siyo ya kweli.

Madai kwenye tafiti hiyo yanaonekana kuwa sio kweli baada ya sehemu ya tafiti hiyo kusema “Preprints are preliminary reports of work that have not been certified by peer review. They should not be relied on to guide clinical practice or health-related behavior and should not be reported in news media as established information.”

Ujumbe huo unamaanisha “Machapisho yasiyo rasmi, yasitiliwe maanani na yasitumike na vyombo vya habari kama taarifa rasmi,”

Kwa mantiki hiyo, uvaaji wa miwani hakuweki salama dhidi ya Corona.


Zinazohusiana:


Watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapaswa kutumia taarifa sahihi kutoka machapisho yaliyorasimishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kujikinga na COVID-19.

Baadhi ya tahadhari zinazopendekezwa za kujikinga ni kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara, kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima. 

Hata hivyo, WHO na jumuiya za kimataifa zimepiga hatua kudhibiti ugonjwa huo kwa kuanza kutoa chanjo mbalimbali chini ya programu maalum ya COVAX.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV

Ni changamoto gani zinawakabili vijana wa kitanzania kwa sasa ?

Ni changamoto gani zinawakabili vijana wa kitanzania kwa sasa ?

Nukta TV

Akili Unde (AI) ni suluhu ya habari za uzushi ?

Akili Unde (AI) ni suluhu ya habari za uzushi ?

Nukta TV