Ufinyu wa fedha za maendeleo wapunguza bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa asilimia 3

May 28, 2024 1:55 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Yafikia Sh241 bilioni kutoka Sh247.9 bilioni.
  • Kamati ya NUU yasema ufinyu wa bajeti ya maendeleo utaathiri ukarabati wa majengo ya balozi nje ya nchi.

Dar es Salaam: Serikali imepunguza zaidi ya Sh6.9 bilioni kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika mwaka 2024/25 huku sababu ikitajwa kuwa ni kupungua kwa fedha za miradi ya maendeleo.

Fedha hizo zimepungua kwa asilimia 3, kutoka Sh247.9 bilioni iliyoidhinishwa katika  mwaka wa fedha 2023/24 hadi Sh241 bilioni kwa mwaka ujao wa fedha utakaoanza Julai, 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, aliyekuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/25 leo Mei 28, 2024 bungeni jijini Dodoma, amesema  kuwa, asilimia 95 ya fedha hizo ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, yakijumuisha mishahara na matumizi mengineyo.

“Mheshimiwa Spika, kati ya fedha hizo, Sh229.4 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo ndani yake Sh210.9 bilioni ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, na Sh18.5 bilioni ni kwa ajili ya mishahara. Aidha, Serikali imetenga kiasi kinachobaki cha Sh11.6 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo” amesema Waziri Makamba.

Fedha hizo za maendeleo zilizotengwa kwa mwaka 2024/2025 ni asilimia 4.8 ya bajeti nzima ya wizara.


Soma zaidi:Siku ya Mazingira duniani kufanyika kwa namna yake Tanzania


Wakati bajeti hiyo ikishuka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama(NUU) imebaini kuwa kushuka kwa bajeti ya wizara hiyo kwa  mwaka 2024/25 kumechangiwa na kupungua kwa fedha za miradi ya maendeleo.

Joseph Tadayo Mbunge wa Mwanga (CCM) aliyekuwa akiwasiliisha maoni ya kamati hiyo kwa niaba ya mwenyekiti wake Vita Kawawa amesema fedha hizo za Miradi ya maendeleo zimepungua kwa asilimia 34 kulinganisha na bajeti iliyotengwa 2023 2024 licha ya uhitaji mkubwa wa fedha uliopo katika wizara hiyo.

“Tathimini inaonesha kuwa wizara hii bado inahitaji kufanya ukarabati wa majengo na nyumba za ubalozi ambazo zimechakaa hivyo kuathiri taswira ya nchi yetu katika medani za kidiplomasia, matarajio ya kamati ilikuwa ni kuona bajeti ya maendeleo ikiongezeka,” amesema Tadayo.

Aidha, uchambuzi wa kamati pia ulibaini kuwa fedha za maendeleo zinazotengwa na wizara hiyo hazijumuishi gharama za kubadili fedha katika nchi miradi inapotekelezwa jambo linalopeleka fedha hizo kutokujitosheleza.

Vipaumbele vya wizara 2024/25

Waziri Makamba amewaambia wabunge kuwa kwa mwaka 2024/25 wizara yake itatekeleza vipaumbele vitano ikiwemo kuratibu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi ili kuchochea uwekezaji, utalii na biashara pamoja na kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Vingine ni Kuendelea kuimarisha uratibu na ushirikiano wa uwili pamoja na ushirika wa Tanzania katika jumuiya na mashirika ya kikanda na kimataifa ili kulinda maslahi ya Taifa pamoja na kustawisha diplomasia ya kisasa na kujenga uhusiano wa karibu na nchi washirika,” ameongeza Waziri Makamba.

“Kuongeza ushawishi wa Tanzania kwa nchi nyingine katika masuala mtambuka, kwenye jumuiya na mashirika ya kikanda na kimataifa, Kushiriki kwenye jitihada za kikanda na kimataifa za kudumisha amani, ulinzi na usalama” ameongeza Makamba 

Pia wizara itaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi, kuimarisha utawala bora na rasilimaliwatu pamoja na kutekeleza miradi ya ujenzi, ununuzi na ukarabati wa majengo ya ofisi, makazi ya watumishi na vitega uchumi katika balozi za Tanzania na makao makuu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV