Serikali yapandisha bajeti Wizara ya Mambo ya Ndani kwa Sh357 bilioni

May 26, 2025 7:14 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Yaongezeka kwa Sh357.16 bilioni kulinganisha na ile ya mwaka 2024/25.
  • Kamati yasema matumizi yaliyowasilishwa yasipoidhinishwa na Bunge yatakwamisha miradi ya maendeleo.

Dar es Salaam. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeliomba Bunge liidhinishe Sh2.06 trilioni katika mpango wake mpya wa mapato na matumizi kwa mwaka 2025/26 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya Sh357 bilioni kutekeleza majukumu yake ikiwemo ikiwemo kuboresha masuala ya haki jinai.

Fedha hizo zimeongezeka kwa asilimia 21, kutoka Sh1.71 trioni iliyoidhinishwa katika mwaka wa fedha wa 2024/25. 

Innocent Bashugwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amesema bungeni leo Mei 26,2025 kuwa kati ya fedha inayoombwa Sh701 bilioni ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

“Kati ya fedha hizo, Sh950 bilioni ni mishahara na Sh415 bilioni ni fedha za miradi ya maendeleo,” amesema Bashungwa jijini Dodoma.

Bajeti ya mishahara imeongezeka kwa Sh79.89 bilioni sawa na asilimia 9.18 ukilinganisha na Sh 870.43 bilioni iliyoidhinishwa 2024/2025.

Katika fedha za miradi ya maendeleo Sh388.6 bilioni ni fedha za ndani na Sh26.53 bilioni ni fedha za nje.

Baadhi ya wageni waliopata fursa ya kudhuria vikao vya Bunge leo Jijini Dodoma.Picha/Bunge la Tanzania.

Fedha hizo za maendeleo, zimeongezeka kwa Sh125.45 bilioni sawa na ongezeko la asilimia 43.3 ikilinganishwa na kiwango cha Sh289.7 bilioni kilichopangwa mwaka 2024/2025. 

Katika mwaka wa fedha <a href="http://<!– wp:paragraph –> <p>Katika mwaka wa fedha 2025/2026, wizara imepanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuendelea kudumisha usalama wa raia na mali zao, kuboresha na kujenga miundombinu ya ofisi na makazi kwa ajili ya maafisa, wakaguzi na askari wa vyombo vya usalama. </p> 2025/2026, wizara imepanga kutekeleza vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuendelea kudumisha usalama wa raia na mali zao, kuboresha na kujenga miundombinu ya ofisi na makazi kwa ajili ya maafisa, wakaguzi na askari wa vyombo vya usalama. 

Aidha, Wizara imelenga kuimarisha huduma za uhamiaji kwa njia ya mtandao, sambamba na utekelezaji wa zoezi la usajili na utambuzi wa watu walio chini ya umri wa miaka 18.

Licha ya bajeti ya wizara kupaa kwa asilimia 21 Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeionya Serikali juu ya ufinyu wa fedha za maendeleo unaosababisha baadhi ya miradi kukwama hivyo kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Matumizi yaliyowasilishwa yasipoidhinishwa na Bunge kwa kiasi hicho au kwa nyongeza zaidi majukumu ya wizara hii yatakuwa mashakani na shughuli za umma nchini zitaingia matatani,” amesema Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Vita Kawawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks