Twitter yafungua fursa ya kukuza “brand” za wafanyabiashara

September 25, 2019 11:47 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Iko mbioni kuanzisha jukwaa litakalowakutanisha wadau wa biashara na matangazo.
  • Litatumika kushauriana na kutafuta njia bora za kukuza brand za biashara
  • Twitter bado hawajatoa tamko rasmi ni lini litaanza kufanya kazi. 

Kama wewe ni mfabiashara na umekuwa ukitumia mtandao wa Twitter kutangaza bidhaa na huduma, basi una kila sababu ya kutabasamu, kwa sababu mtandao huo unakupeleka katika hatua ya mafanikio zaidi.

Mtandao huo uko mbioni kuanzisha jukwaa jipya la “Twitter Next” ambalo linawakutanisha wadau na wabia wa biashara duniani kujadili na kushauriana njia bora za kukuza biashara na “brand” zao.

Kwa mujibu wa mtandao wa Social Media Today, Twitter inaungana na watengeneza maudhui na warusha matangazo ili kutafuta namna bora ya kufaidika na jukwaa hilo ambalo ni maalum kwa watu wenye nia kukuza “brand” zao. 


Zinazohusiana:


Huenda huduma hiyo mpya ya Twitter itawasaidia wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa teknolojia ya kisasa na yenye uwezo mkubwa wa kupata uchaguzi mpana wa jinsi ya kuwafikia wateja ambao ni muhimu katika kuwaingizia kipato.

Hata hivyo, Twitter  hawajatoa tamko rasmi la jukwaa hilo na lini litaanza kufanya kazi kwa watumiaji wake. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV