Facebook yafanya maboresho utafutaji wa bidhaa mtandaoni

September 14, 2018 3:44 pm · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Maboresho hayo yatawarahisishia watumiaji wa mtandao huo kupata haraka bidhaa wanazotafuta kutoka sehemu yoyote ndani ya mtandao huo.
  • Ni hatua muhimu katika kukuza teknoloja ya mawasiliano na ushindani wa mitandao ya kijamii. 

Dar es Salaam. Kila siku ni siku ya mabadiliko ya kiteknolojia. Kampuni zinazotuoa huduma ya mitandao ya kijamii zimejidhatiti kuwapa wateja wao taarifa na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu, lengo likiwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kuendelea kuwepo kwenye ushindani wa soko.

Mtandao wa Facebook hauijabaki nyuma katika kuwapatia wateja wake kila wanachokitaka. Safari hii imekuja na mabaresho ya kuwasaidia watumiaji wa mtandao huo wanaotatizwa kupata matokeo wanayoyataka pindi wanapotafuta taarifa au bidhaa ndani ya mtandao huo. 

Maboresho hayo yamefanyika katika sehemu ya kutafutia vitu (search engine) ambapo mtumiaji atapata taarifa za picha, sauti, maandishi hata video zinazopatikana ndani ya mtandao huo kwa haraka zaidi; ni tofauti na awali baadhi ya taarifa zilikuwa hazipatikani kulingana na mahitaji ya mtu binafsi.

Huo ni mwanzo wa safari ndefu ya kuifanya Facebook iwe ya kuaminika zaidi. Maono ya baadaye ni kuimarisha mfumo wa kupata taarifa na kudhibiti zisizozingatia maadili katika mtandao huo.

Facebook imeweza kutoa moja ya dhumuni lao la kuweka kipengele hicho ili kusaidia watu mbalimbali katika kuinua biashara zao kwa kutafuta bidhaa na kuwawezesha kuona matokeo ya wateja wanaohitaji au kununua biadhaa husika.  Pia itaonyesha muda ambao unatumika kutafuta bidhaa na matumizi yake. 

Kwa mabadiliko yanayotokea katika matumizi ya mitandao ya kijamii ni dhahiri, maisha ya watu yanazidi kuboreshwa kwa kuondokana na changamoto ambazo zisingetatuliwa bila uvumbuzi wa teknolojia ya mawasiliano na habari.

Muonekano mpya wa kipengele kinachotumika kutafuta bidhaa au taarifa.|TechViral.

Enable Notifications OK No thanks