TLS,  wadau wa maendeleo waomba kukutana na Rais Samia

August 26, 2025 4:14 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Wasema majadiliano na Rais ni muhimu kulinda amani, haki na mshikamano wa kitaifa.

Dar es Salaam. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeomba kukutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ili kuwasilisha maoni ya wadau mbalimbali kuhusu changamoto zinazopaswa kutatuliwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.

Hatua hiyo huenda ikasaidia kuongeza ushiriki wa makundi mbalimbali ambayo yamekuwa yakilalamikia baadhi ya vitu ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi aliyekuwa akizungumza leo Agosti 26, 2025 na wanahabari jijini Dar es Salaam amesema tayari wamewasiliana na Ofisi ya Rais kwa ajili ya kuwasilisha maazimio hayo.

“Lengo letu TLS kwenda kwa Rais hatuendi ‘kudictate’ tunaenda kwa unyenyekevu kumwambia Rais wewe ni Rais wa Tanzania, sio wa Chama cha Mapinduzi (CCM), sio wa wabunge, sio wa vyombo vya ulinzi na usalama…

…Huyo ni Rais wetu sote. Tunapokuwa na hoja kama hizi tunawasilisha kwake tupate ‘forum’ ya kukaa naye atusikilize,” ameeleza Mwabukusi.

Rais wa TLS Boniface Mwabukusi akizungumza na wanahabari. Picha/ Tanganyika Law Society.

Hata hivyo, Mwabukusi amebainisha kuwa changamoto zinazojitokeza wakati wa uchaguzi zinapaswa kuwa za kimsingi na siyo zinazotokana na wale wanaohusika na uratibu wa uchaguzi.

Kwa mujibu wake, TLS imekuwa mstari wa mbele kuratibu mazungumzo ya amani yaliyojumuisha taasisi za dini, vyama vya siasa, watu mashuhuri pamoja na asasi za kiraia, ili kujadili haki, amani na utulivu kabla na baada ya uchaguzi.

TLS imeratibu mazungumzo ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu (2025)… Lengo kuu lilikuwa ni kujadili masuala ya haki, amani na utulivu kabla, wakati na baada ya uchaguzi kwa kuzingatia changamoto na fursa zilizopo kwenye mifumo ya kisheria, kitaasisi na kijamii,”  ameongeza Rais wa TLS.

Aidha, TLS imesisitiza kuwa itaendelea kuwa daraja la haki kwa njia ya mazungumzo na maelewano bila kumlazimisha au kumpendelea mtu na kwamba mazungumzo na Rais yanalenga kurejesha imani ya wananchi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa shirikishi, huru na wa haki.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.