Serikali yazindua mfumo mpya wa kielektroniki kupunguza changamoto za ajira nchini

August 22, 2025 2:30 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Mfumo huo utasaidia upatikanaji wa taarifa za kazi na mwenendo wa ajira nchini.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imezindua mfumo mpya Mfumo wa Kieletroniki wa Taarifa za Soko la Ajira (NLMIS) unaotajwa kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa ajira nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Ridhiwani Jakaya Kikwete aliyekuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, leo Agosti 22, 2025, amesema kuwa utasaidia kutatatua changamoto zilizokuwepo awali ikiwemo ugumu na mtawanyiko wa taarifa za ajira zilikuwa zimetawanywa katika taasisi  mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kikwete, ukosefu wa taarifa hizo ulisababisha urasimu, ukosefu wa jukwaa la kitaifa la pamoja na pengo kubwa la ujuzi na unaotolewa na vyuo vya elimu na mafunzo kwa uhitaji wa soko la ajira, mambo ambayo kwa ujumla wake yalichangia kuongezeka kwa changamoto za ukosefu wa ajira kwa wahitimu na ukosefu wa takwimu za Serikali zitakazosaidia upangaji mzuri wa mikakati ya ajira. 

“Kupitia mfumo huu Serikali ina lengo la kuweka jukwaa la kidijitali litakalokusanya na kuchambua na kusambaza taarifa za soko la ajira kwa uwazi na ufanisi ukiunganishwa na wadao wote muhimu wakiwepo waajiri, waajiriwa, wahitimu wa vyuo vikuu na mashirika ya ajira,” amesema Kikwete.

Aidha, Kikwete amesema kuwa mfumo huo ambao unapatikana kupitia tovuti ya www.jobs.kazi.go.tz/portal  utasaidia Serikali kupanga sera, mikakati madhubuti, na kurekebisha mitaaala ili iendane na mahitaji ya soko na kutoa fursa kwa watu wanaotafuta ajira kupata taarifa sahihi kwa wakati na njia rahisi zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mary Ngelela Maganga amesema kuwa uundaji wa mifumo hiyo umejumuisha wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri ili kuhakikisha uandaaji unakuwa shirikishi.

“Mifumo hii itaongeza tija kwa Serikali na wadau ambao ndio watumiaji wa miongozo na mifumo hii,” amebainisha Maganga.

Huenda mfumo huo ukapunguza changamoto ya ajira hususani kwa kundi la vijana wenye uwezo wa kufanya kazi ambao Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 inawataja kuwa asilimia 34.4

Mbali na NLMIS, Serikali pia imezindua mfumo mwingine wa kidijitali wa Usimamizi wa Mashauri ya Usuluhishi (Online CAS Management System) unaolenga kupunguza gharama na muda unaotumika na wadai wa ajira kusafiri umbali mrefu kufuata haki zao.

Kwa mujibu wa Kikwete, mfumo huo mpya utawawezesha wananchi kutumia muda mwingi zaidi kwenye shughuli za uzalishaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Uzinduzi wa mifumo hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika mkoani Singida Mei1, mwaka huu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV