Thamani ya mauzo soko la hisa Dar yapaa mara tatu

October 5, 2019 8:12 am · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Thamani ya mauzo ya wiki nzima katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imepanda zaidi ya mara tatu hadi Sh1.17 bilioni kutoka Sh357.4 milioni iliyorekodiwa juma lililopita.
  • Wachambuzi waeleza soko hilo huenda likafanya vizuri zaidi siku zijazo kutokana na matarajio ya matokeo ya robo ya tatu ya mwaka ya benki.

Dar es Salaam. Thamani ya mauzo ya wiki nzima katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imepanda zaidi ya mara tatu hadi Sh1.17 bilioni kutoka Sh357.4 milioni iliyorekodiwa juma lililopita huku wachambuzi wakitabiri mwenendo chanya siku zijazo.

Uchambuzi wa soko kwa wiki iliyoanzia Septemba 30 hadi Oktoba 4 uliofanywa na kampuni ya udalali ya masoko ya mitaji na dhamana, Zan Securities, unabainisha kuwa thamani ya mauzo katika soko hilo iliongezeka kwa asilimia 228 kutoka yale ya wiki iliyopita.

Wiki za DSE hujumuisha siku za kazi pekee yaani Jumatatu hadi Ijumaa.

Mauzo ya soko la hisa yamekuwa na mwenendo wa kupanda na kushuka ambapo wiki jana thamani ya mauzo ilishuka hadi Sh357.43 milioni kutoka takriban Sh505 bilioni iliyorekodiwa katika wiki iliyoishia Septemba 20.“TBL (Kampuni ya bia Tanzania) ndiyo kampuni iliyochagiza zaidi ongezeko la mauzo hayo baada ya kurekodi asilimia 79.37 ya thamani ya mauzo yote ikifuatiwa na benki ya CRDB yenye asilimia 16.04,” imesema taarifa iliyotolewa leo (Oktoba 4, 2019) na Mtendaji Mkuu wa Zan Securities, Raphael Masumbuko.


Zinazohusiana: 


 Masumbuko amesema soko la mitaji lilionyesha matumaini makubwa baada ya thamani ya mauzo kuvuka kikomo cha bilioni.

“Matokeo ya kifedha ya robo ya tatu ya mwaka ya taasisi za kibenki yanatarajiwa kutoka siku chache zijazo…tunaamini kuwa yatachochea kwa kiwango kikubwa utendaji wa soko,” amesema Masumbuko katika utabiri wa hali ya soko wiki ijayo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nyumba nafuu Dar zinavyowasukuma wakazi kwenye maeneo hatarishi

Nukta TV

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Haya ndio maajabu ya iPhone Duo simu mpya kutoka Apple

Nukta TV

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Kitakachotokea IGP, CDF na DCI wasipofika mahakamani kesi ya Lissu

Nukta TV